TAZAMA FULL VIDEO BOFYA LINK HII
Na Matukio Daima media
UPANDE wa Jamhuri katika Kesi ya mauaji inayowakabili watuhumiwa watano akiwemo diwani wa kata ya Nyanzwa Boniphace Yohana Ugwale katili ,mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Chama Cha mapinduzi (CCM )wilaya ya Kilolo Hedikosi Gwerino Kimwaga na wenzao watatu imesoma upya shitaka hilo kwa kuwaunganisha watuhumiwa wote watano.
Watuhumiwa wote kwa pamoja walifikishwa Mahakamani hapo leo majira ya saa 3:47 asubuhi kwa gari Mbili Wao wakiwa kwenye gari aina ya Land Cruiser yenye namba za usajili PT 1909 huku gari aina ya Land Cruiser yenye namba KM 91 MS -GP ikiwa nyuma na askari waliobeba silaha mbali mbali na mabomu ya machozi.
Kwa muda wote kabla ya watuhumiwa hao kufikishwa Mahakamani hapo wananchi mbali mbali wakiwemo ndugu wa marehemu ,viongozi wa Jumuiya za CCM na Makada wa Vyama mbali mbali na wasio na vyama walijitokeza kusikiliza Kesi hiyo tofauti na Siku ya kwanza ambayo waliofika ni ndugu wa watuhumiwa Pekee ambao hawakuzidi 10.
Watuhumiwa wamefikishwa Mahakamani Jana Mbele ya hakimu mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Iringa Rehema Mayagilo kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa katibu wa Chama Cha mapinduzi (CCM)wilaya ya Kilolo Christina Nindi Kibiki ni pamoja Kefa John Wales,Silla Johnson Kimwaga,Boniphace Yohana Ugwale katili ,Willy Gerald Chikweo na Hedikosi Gwerino Kimwaga.
Mwendesha mashitaka upande wa Jamhuri Sauli Makori aliiambia Mahakamani hiyo kuwa kwa kuwa mshitakiwa namba Moja katika Kesi hiyo Kefa John Wales alifikishwa Mahakamani hapo na kusomewa shitaka hilo Pekee yake kabla ya watuhumiwa wengine wanne kusomewa wiki shitaka hilo anaimba kusoma upya maelezo ya kosa kwa watuhumiwa wote watano .
Akisoma upya maelezo ya Kesi hiyo ya Jinai namba 34404 ya mwaka 2024 kosa la mauaji kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo la mauaji Novemba 12 mwaka 2024 katika Kijiji Cha Ugwachanya wilaya ya Iringa Vijijini.
Hata hivyo alisema upelelezi wa Kesi hiyo bado haujakamilika .
Hata hivyo hakimu katika Kesi hiyo alisema watuhumiwa hawapaswi kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina Uwezo wa kusikiliza Kesi hiyo.
Katika Kesi hiyo washitakiwa wote watano wanatetewa na mawakili wawili Barnabas Nyalusi na Neema Chacha kutoka kampuni ya mawakili ya BLS ATTORNEYS &Partner
Hata hivyo baada ya Kesi hiyo kuahirishwa na wakati watuhumiwa hao na wengine wakipandishwa kwenye gari Kuelekea magereza ya mkoa wa Iringa baadhi ya watuhumiwa wa Makosa mengine walisikika wakipaza Sauti kuwapongeza waandishi wa habari kwa kutimiza wajibu Wao .
"Kazi nzuri kazi nzuri waandishi pigeni kazi "ni Maneno ya watuhumiwa wengine walikupandishwa gari Moja na watuhumiwa hao wa mauaji
0 Comments