JUMLA ya Wapiga Kura wapya 121,187 wanatarajiwa kuandikishwa kwenye uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura Katika Mkoa wa Lindi
Hayo yamebainishwa na Kaimu mkurugenzi wa tume ya huru Taifa ya uchaguzi Giveness Aswile wakati alipokuwa anazungumza Katika mkutano wa tume na wadau wa uchaguzi wa kuhusu uboreshaji wa daftari la wapiga kura uliofanyika Katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi huko Mkoani Lindi
Aswile Amesema kuwa Wapiga Kura hao wapya ni ongezeko la la asilimia 18.7 ya wapiga kura 645,644 waliopo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura hivyo mkoa wa Lindi unatarajia kuandikisha wapiga 768,641. Kwa kutumia vituo 1308 vilivyopangwa
Awali akifungua mkutano huo, makamu Mwenyekiti wa tume huru ya taifa ya uchaguzi, Mheshimiwa Jaji (R) ( MST.) Mbarouk Mbarouk aliwahasa wawakilishi hao kuendelea kutoa Elimu kwa wananchi wengine kujitokeza kujiandikisha Katika Daftari la kudumu muda utakapofika
Hata hivyo Jaji Mbarouk alisema kuwa ni kosa la jinai mwananchi kujiandikisha zaidi ya mara moja na endapo ukibainika unaweza fungwa jela miezi sita au miaka miwili ili kujiepusha na kadhia hiyo wananchi wanapaswa kujiandikisha mara moja tu.
"Kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 10 Cha sheria ya Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani Na.1 ya mwaka 2024,wafuatao hawana sifa za kuandikishwa kwenye Daftari,Iwapo mtu yupo chini ya kiapo Cha utii wa nchi nyingine tofauti na Tanzania,Hana akili timamu"
Pia Jaji Mbarouk alisema mwananchi yoyote yule aliyewekwa kizuizini kama muhalifu mwenye ugonjwa wa akili,Amewekwa kizuizini kwa ridhaa ya Rais,Ametiwa hatiani kwa kosa ambalo adhabu yake ni kifo na anatumikia kifungo kwa kosa ambalo adhabu yake inazidi miezi sita iliyotolewa na mahakama.
0 Comments