Baadhi ya Walimu Wenye changamoto mbalimbali kutoka Maneno mbali mbali ya mkoa wa Iringa wakiwa katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa Kukutana na timu ya Samia Teacher Mobile Clinic
NA MATUKIO DAIMA MEDIA
CHAMA cha walimu Tanzania (CWT) kimesema kitashughulika na mtu mmojammoja atakayebainika kuwavuruga walimu kupitia mambo ya kisiasa yanayosababisha kuwavuruga walimu na kuwagawa katika makundi.
Makamu mwenyekiti wa CWT Taifa Suleiman Ikomba alitoa onyo hilo Leo katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa wakati wa zoezi la usikilizaji na utatuzi wa changamoto mbalimbali za walimu kupitia kikosi kazi Cha SAMIA TEACHERS MOBAILE CLINIC.
Alisema kuwa viongozi wa CWT hawatawavumilia watu wanaotaka kuwavuruga walimu kupitia siasa.
Ikomba alisema kuwa Jamii inatakiwa kuacha kuingiza siasa katika sekta ya elimu hususani kwa walimu na kusababisha kuwagawa walimu hao katika makundi hali itakayopelekea walimu kutofanya kazi zao kwa weledi kwa kuwaza migogoro itakayokuwa imazalishwa.
Alisema kuwa walimu wanakazi kubwa ya kuhakikisha walimu wanatoa elimu bora kwa vijana/ wanafunzi hivyo wakianza kuvurugwa kisiasa kutaanza kuwagawa makundi jambo ambalo halipaswi kufumbia macho kwakuwa mwalimu akivurugwa inakuwa imevurugwa elimu kwa ujumla.
“Yapo madhara makubwa sana walimu wanapogawanyika naka kama kunamtu anataka kuwavuruga alimu atakuwa ameivuruga nchi yetu hatutakaa kimya kuona mtu anaivuruga CWT ikumbukwe kuwa CWT sio chombo cha serikali ni chombo cha Walimu .
Alisema kama kuna mtu anawachezea waalimu atakuwa amewasababishi watoto maana atakuwa amewakosesha wanafunzi kupata elimu kwa kuwa walimu watakuwa wanashughulukia matatizo ambayo atakuwa amesababishiwa na mwananchi mmoja.
Alisema mwalimu mmoja anafundisha watoto zaidi ya 200 hivyo kumosea mwalimu huyo ni sawa nakuwakosea wanafunzi zaidi ya 200 kwa kukosa vipindi kwaajili ya mtu mmoja ambaye yupo kwa maslahi yake binafsi.
Alisema kuwa haikwepeki kwa walimu kufanya kazi kwa kutekeleza ilani ya chama tawala kwa kuwa wao ni kama watumishi wengine katika serikali inayoongozwa na chama cha mapinduz CCM.
“ sisi walimu ni kama watumishi wengine ambao tunatekeleza ilani ya CCM kwa kua ndio walioshika dola na kama kutakuja kuwa na chama chochote kitashika dola tutekeleza ilana yake lakini sio kuwavuruga walimu hawa ambao wapo kuhakikisha vijana wetu wanapata elimu bora”alisema Ikomba
Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa Iringa Doris Kalasa akifungua zoezi hilo la SAMIA TEACHERS MOBAILE CLINIC alisema kuwa walimu wanatakiwa kuungana kwa umoja wao na kama wanachangamoto za kiuongozi ni vyema wakaziwasilisha kwa viongozi wao katika chama cha walimu na kama itashindikana ndipo wawasilishe changamoto zao ngazi ya juu.
Akizungumzia zoezi hilo la kutatua kero za walimu Kalasa alisema kuwa muitikio wa walimu umeku ni mkubwa hivyo inamaanisha walimu walikuwa na kero nyingi ambazo kliniki hii ya Rais Samia itakuwa ni suluhishi.
“kwa mwitikio huu wa walimu katika zoezi la kutatuliwa kero zao na uhakika asilimia 95 ya walimu watafikiwa na watasikilizwa sina mashaka na timu hii iliyofika hapa mkoani kwetu kwani ni watu makini na weledi na ni watu walioaminiwa na serikali”alisema Kalasa.
Alisema kuwa CWT wanatakiwa kupongezwa kwa ubunifu mzuri wa kusikiliza na kutatua kero na changamoto za walimu kupitia kliniki ya Rais Samia iliyolenga kutatua changamoto za walimu hao.
Alisema kuwa kliniki hiyo inayotatua changamoto za walimu itawafanya walimu kufanya kazi zao kwa utulivu katika maeneo ya kazi ma hivyo kuongeza ari na motisha ya utekelezaji wa majukumu yao ili hatimaye kuongeza ufaulu katika masomo ya wanafunzi.
Mwenyekiti wa chama cha walimu Tanzania CWT mkoa wa Iringa mwalimu Gaur Mgalula alisema kuwa watumishi wa idara ya rasilimali watu wamekuwa wakiwatoa walimu katika makato ya chama hali inayosababisha walimu kukosa kuhudumiwa na hiyo hutokana na maslahi yao binafsi.
Alisema walimu CWT imeendelea kuwahudumia walimu wote katika changamoto zao hataka walijitoa kwenye chama cha walimu hivyo wanatakiwa kuwa huru hata wanapofikiwa na huduma hii ya utatuzi wa kero za walimu.
Alisema walimu wanatakiwa kukitunza na kukisema vizuri chama cha walimu kwa kuwa kinafanya kazi ya kutetea walimu hata walio nje ya chama hicho japo watumishi wa idara ya rasilimali watu wamekuwa wakiwatoa walimu katika makato ya chama.
Aidha Mgalula licha ya kuwapongeza walimu kwa kufika kwa wingi .
Mgalula alisema kuwa changamoto za walimu zitakazo sikilizwa ni pamoja na upandishwaji wa vyeo, mabadiliko ya miundo ya utumishi, madai ya malimbikizo ya mishahara na mishahara kutokuhamishwa baada ya uhamisho.
Kwa upande wenyekiti mstaafu wa wa chama cha walimu CWT mkoa wa Iringa, Mwalimu Stanslaus Mhongole, alisema kuwa kliniki ya mama samia inalengo la kuponya vidonda vya walimu mbalimbali waliokuwa wanakero nyingi.
Alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa CWT hakujawahi kuwa na cliniki kama hiyo ya kusikilizwa na kutatuliwa kero zao muda huo huo hivyo walimu katika maeneo yote nchini wachangamkie fursa hiyo ya kwenda kutatuliwa kero zao.
Walimu kutoka maeneo mbalimbali mkoni Iringa na nje ya mkoa wa Iringa walisema kuwa ni bahati kubwa kwao kukutana na timu hiyo ambayo katika utumishi wao ni hakujawahi kuwepo kwa tume hiyo.
Walisema kuwa wamekuwa na changamoto nyingi katika kazi zao lakini ujio wa cliniki hiyoumekuwa nifaraja kubwa kwao kwani wanauhakika changamoto zao.
Alisema timu hiyo ya Samia Teacher Mobile Clinic imehusiaha watalamu kutoka CWT,Ofisi ya Rais (OR)Tamisemi ,Ofisi ya rais UTUMISHI ,Wizara ya elimu ,tume ya utumishi wa walimu (TSC) pamoja na benk ya Walimu (MCB)
0 Comments