Header Ads Widget

UTEKELEZAJI WA MIRADI WAGUSA KILA MTANZANIA -CCM KIGOMA

Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma Jama Tamim na viongozi wa CCM mkoa Kigoma wakielekea  eneo la   mkutamo wa hadhara mjini Kasulu ambapo walitangaza azma ya kuunga mkono azimio la mkutano mkuu wa CCM Rais Samia kuwa mgombea pekee wa ccm katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu
 Na Fadhili Abdallah,Kigoma

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoa Kigoma kimesema kuwa utekelezaji miradi inayogusa Maisha ya kila siku ya Mtanzania ndiyo chachu kubwa ya wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM Taifa kuazimia kumuunga mkono Raisi Samia Suluhu Hassan  kuwa mgombea pekee wa chama hicho atakayechukua fomu katika uchaguzi mkuu ujao.


Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma, Jamal Tamim alisema haayo akizungumza katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika mjini Kasulu jana ukiwa na azma ya kumuunga mkono Raisi Samia kuwa Mgombea uraisi wa Tanzania, Dk.Hussein Ally Mwinyi kuwa mgombea urais Zanzibar na Dk.Emanuel Nchimbi kuwa mgombea Mwenza wa Mgombea Urais wa Tanzania.

Tamim alisema kuwa kwa sasa Tanzania inatekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ambayo kila mmoa inagusa moja kwa moja Maisha ya wananchi wa kawaida wa kipato cha chini ikiwemo miradi ya umeme, miradi ya afya, miradi ya elimu, kiradi ya maji, uimarishaji wa miundo mbinu ya usafiri na usafirishaji, uwezeshaji wananchi kiuchumi na mradi wa reli iendayo kasi (SGR) ambayo imeoyesha kula mafanikio makubwa katika mapinduzi ya usafiri nchini.

“Kigoma Mama Samia ameleta Zaidi ya trilioni 11.9 na miradi inatekelezwa ikiwemo ujenzi wa meli mpya katika ziwa Tanganyika ambazo ni kiungo muhimu cha uchumi kwa wafanyabiashara ziwa Tanganyika, umeme wa gridi ya Taifa ambao umefanya Kigoma kuondokana na umeme wa majenereta hivyo CCM Kigoma haina sababu ya kutomuunga mkono na hivyo kuazimia kumpa miaka mitano tena,”Alisema Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa Kigoma.

 Kwa upande wake Menyekiti wa Jumuia ya Wanawake (UWT) mkoa Kigoma, Agripina Buyogela alisema kuwa Raisi Samia ameonyesha kwa vitendo jinsi anavyowajali wanawake ikiwemo kuwaletea mradi wa gesi safi ya kupikia aambayo imekuwa maono yake makubwa katika kuwakomboa wanawke na adha za jikoni.

Buyogera alisema kuwa wakiwa wajumbe wa mkutano mkuu kwa niaba ya wanawake wa Tanzania hawana budi kuuunga mkono azimio la kumpa Raisi Samia miaka mitano mingine ili atomize lengo la azma yake katika kuwatumikia watanzania.

Baadhi ya wananchi wa mjini Kasulu wakiongea na waandishi wa Habari baada ya mkutano huo akiwemo Laurent Masunzu mkazi wa eneo la Mwilanvya Kasulu mjini alisema kuwa miradi ya kimkakati inayotekelezwa chini ya utawala wa Raisi Samia imekuwa chachu ya ukuaji wa maendeleo kwa wakazi wa mkoa huo ambao awali walilazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za kijamii mbali na maeneo yao ya makazi.

Masunzu alieleza kuwa  miradi hiyo imebadili Maisha yao kwa haraka kutokana na juhudi za serikali ya awamu ya sita ambapo kwa sasa huduma za msingi za kibinadamu ikiwemo huduma za afya, elimu,maji, umeme wa uhakika na miundo mbinu bora ya barabara imewezesha wananchi hao kuanza kupiga hatua za kiuchumi katika kuinua Maisha yao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI