Na Fadhili Abdallah,Kigoma
CHAMA Cha Mapinduzi CCM mkoa Kigoma kimesema kuwa maboresho makubwa ya miundo mbinu ya barabara na miundo mbinu ya usafiri na usafirishaji imeleta tija kubwa katika shughuli za kiuchumi za wananchi wa mkoa Kigoma.
Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma,Jamal Tamim alisema hayo katika uzinduzi wa miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM uzinduzi uliofanyika kwenye kijiji Kalago wilaya ya Uvinza Mwambao wa kusini wa ziwa Tanganyika mkoani Kigoma.
Jamal alisema kuwa mfano wa uboreshaji wenye tija uliofanyika mkoani Kigoma ni pamoja na barabara ya Simbo hadi Kalya ambayo ujenzi wake umerahisisha usafirishaji wa mazao kwenda sehemu mbalimbali nchini hivyo kufungua soko na kuongeza uchumi wa wananchi wa enjoy hilo.
Katika uzinduzi huo Mwenyekiti huyo wa CCM alitembelea ujenzi wa shule ya Sekondari Kalago iliyoanza kwa nguvu za wananchi na sasa imefikia usawa wa boma hivyo kuchangia mifuko 50 ya Cement sambamba na kutoa kiasi cha shilingi laki tank kusaidia ukarabati wa kikosi cha wanajeshi wanaolinda amani mwambao wa kusini wa ziwa Tanganyika ambao makazi yao yaliharibiwa na kuongezeka kwa kina cha maji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuia ya wanawake (UWT) mkoa Kigoma, Agripinq Buyogera alisema kuwa miaka 48 tangu kuzaliwa kwake CCM imesimama pamoja na watanzania katika kuwaletea maendeleo na kuwataka watu wote kupuuza maneno yanayotolewa na wapinzani kwamba miaka zaidi ya 60 ya uhuru serikali ya CCM haijafanya chochote.
Buyogera alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita serikali imetekeleza miradi mikubwa ambayo imeleta maendeleo makubwa mkoani humo miradi ambayo imechochea ukuaji mkubwa wa uchumi mkoani humo.
0 Comments