Na Fatma Ally Matukio DaimaApp
KATIKA kuelekea kutimiza miaka 48 ya Chama cha Mapinduzi (CCM),tangu kuzaliwa kwake, Chuo cha Ufundi Furahika VETA kilichopo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam kimeipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kusimamia vyema ilani ya Chama hicho kwa kupiga hatua katika kukuza Sekta ya Elimu nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa bodi ya Chuo hicho Ngwenje Mohamed amesema Sekta hiyo imekuwa Kwa kiwango Cha juu ikilinganishwa na miaka ya huko nyuma kwani sasa shule za kata Kila mahali vyuo vya kati na vikuu vimeongezeka hiyo yote ni jitihada za Chama cha CCM kupitia ilani yake kuhakikisha kila Mtanzania bila kubagua dini Chama ukabila watu wote wanapata elimu.
"Kuelekea maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa chama cha CCM Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan tunaona mengi aliyoyafanya ameendeleza utoaji elimu bure vyuo vya Ufundi Veta navyo vikipewa kipaumbele ili kuibua ujuzi na tafitibalimbali hii inaonyesha kuwa, mazingira ya Elimu nchini Tanzania ni mazuri "amesema Mohamed
Sambamba na hayo amebainisha kuwa ni mambo mengi yamefanyika ikiwemo Sekta ya Afya ujenzi wa Zahanati kuongezeka kwa wataalamu wa Afya madaktari Amesema kuwa tangu kuzaliwa kwa Chama hicho maendeleo ni makubwa ndani ya nchi ya Tanzania ikiwemo sekta ya uchumi unaku kwa kasi hospital, Shule, ambapo zamani wanafunzi walikua wakitumia umbali mrefu lakini sasa hivi kila Kata kuna zipo hata kiwango cha wasomi kinazidi kuongezeka pamoja na kuwepo kwa vyuo na vyuo vikuu nchini.
"Mazingira ya elimu yameboreshwa vizuri, sisi tunatoa elimu bure tena kwa viwango ambapo wanafunzi wetu waliohitimu zaidi ya 700 wamepata ajira katika sehemu mbalimbali, tuna kila sababu ya kuipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi bora na thabiti wa Dkt Samia"amesema
0 Comments