Header Ads Widget

TUMIENI NISHATI SAFI YA KUPIKIA-MHE. KITANDULA

 


Na Anangisye Mwateba-Mlele Katavi


Wakuu wa vyuo vya mafunzo ya uhifadhi nchini wametakiwa kuhakikisha wanatumia nishati safi ya kupikia ikiwa ni maagizo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa taasisi zote za umma zinazohudumia watu zaidi ya 200 kuhakikisha zinatumia nishati safi ya kupikia ili kuepukana na changamoto ya  uharibifu wa Mazingira kwa  ukataji miti kwa ajili ya kuni za kupikia hivyo kusaidia kupambana  na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi.


Wito huo umetolewa na  Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Dunstan Kitandula wakati akihitimisha mafunzo ya mabadiliko ya muundo wa utendaji kutoka wa kiraia kwenda wa Kijeshi kwa askari na maafisa wa Jeshi la Uhifadhi katika chuo cha Mafunzo Mlele mkoani Katavi.


Aidha Mheshimiwa Kitandula aliwakumbusha wakuu wa Taasisi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS), Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro(NCAA), Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA) na Shirika la Usimamizi wa wanyapori Tanzania (TAWA) kuhakikisha wanatenga bajeti kwa ajili ya kushughulikia miundombinu katika chuo hicho ikiwemo kuweka vifaa tiba katika zahanati iliyopo chuoni hapo.


Vilevile Mhe. Kitandula alitumia nafasi hiyo kukemea vitendo vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya askari na maafisa wa jeshi la uhifashi pale ambapo wanatimiza majukumu yao ya ulinzi na utunzaji wa maliasili za misitu na wanyamapori.


“natambua kwamba kumekuwepo na baadhi ya maafisa na askari wasio waaminifu wanaokiuka maadili na miiko ya kazi zao kwa kujihusisha na upokeaji wa rushwa, kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa ukamataji, kushirikiana na majangili katika kuhujumu maliasili za Taifa, natoa rai kwenu wote, afisa na askari yeyote atakayebainika kujihusisha kwa namna moja ama nyingine katika kutekeleza majukumu yake kinyume na sheria, kusaidia kutenda au kufanya uhalifu hatua kali zitachukuliwa dhidi yake” alisema Mhe. Kitandula


Akimkaribisha Naibu wa Waziri, Naibu Katibu Mkuu anayeshighulikia maliasili Kamishina wa Polisi  Benedict Wakulyamba alisema kuwa Maafisa na Askari hao wahitimu moja ya mafunzo waliyopata ni matumizi  bora ya falsafa ya Mhe. Rais ya R4 Maridhiano (Reconciliation), Ustahamilivu (Resilience), Mageuzi (Reforms), na Kujenga upya Taifa (Rebuilding) watakapokuwa wanatimiza majukumu yao katika taasisi zao.










Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI