Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika ( TLS) Wakili Boniface Mwabukusi, amesema watu wana wajibu kujifunza kuongea kwa hoja kuliko kushambuliana, kubaguana kwa misingi ya udini au ukabila, utanganyika au uzanzibari.
Badala ya kuendekeza hayo Mwabukusi amewataka watu mbalimbali kueleza watayofanya kwa watanzania endapo watapata mamlaka ya kuwaongoza.
Mwabukusi amesema hayo januari 13, 2025, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema ni jambo la msingi katika Demokrasia kuheshimu katiba ndani ya vyama na nje ya vyama hata kama kuna uhuru wa maoni lakini uhuru huo usivuke mpaka wa kuingilia falagha, utu, dini, hali za watu bila kuendekeza itikadi zisizo na msingi.
0 Comments