Mashindano hayo ambayo yatashirikisha timu 104 za soka Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani zinatarajiwa kuwania kinyanganyiro hicho kitakachoanzia ngazi ya Kata.
Aidha mbali ya mshindi wa mshindi wa pili atajinyakulia pikipiki na mshindi wa tatu atapata kiasi cha shilingi milioni 1.
Akizindua mashindano hayo kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mtongani Mlandizi Kibaha mdau wa Mpira wa Miguu nchini Haji Manara ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 1 kwa ajili ya mashindano hayo ambayo yameandaliwa na Umoja wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Kibaha.
Michuano hiyo itashirikisha timu kutoka kwenye Kata zote za Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha ikiwa na lengo la kuhamasisha wananchi wakiwemo vijana kujiandikisha na kushiriki kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Manara amesema kuwa amevutiwa na vijana kuandaa mashindano hayo ambayo yanaunga mkono jitihada za Rais Dk Samia Suluhu Hassan kuchangia kwenye michezo ambayo ni ajira na ni sehemu ya kuleta maendeleo nchini.
Kwa upande wake katibu wa hamasa wa UVCCM Kibaha Vijini Godfrey Mwafulilwa amesema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuhamasisha watu kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura na kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa watu kuboresha taarifa zao.
Mwafulilwa amesema kila kata watacheza hatua ya awali na kupata timu 16 bora zitacheza ngazi ya Wilaya na kwenye mashindano hayo hakutakuwa na kiingilio na kila timu itapatiwa jezi na mipira miwili huku zawadi nyingine ni mchezaji bora kipa mfungaji kila mmoja atapata ngao na shilingi 50,000 na timu yenye nidhamu shilingi 100,000.
Naye mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Pwani COREFA Robert Munis amesema kuwa malengo yao ni kuhakikisha mpira Pwani unachezwa kwa kuzingatia taratibu na watashirikiana na wadau wanaoandaa mashindano mbalimbali lengo likiwa ni kuhakikisha vijana wanakuza vipaji vyao kwani soka ni ajira.
Baadhi ya viongozi wa timu hizo wamewashukuru waandaaji wa mashindano hayo ambapo timu za Kujiandikisha na timu oresha taarifa zilitoka sare ya bao 1-1.
0 Comments