Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima App Dodoma
RAIS wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa Kuzindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 toleo la 2023 na Mitaala iliyoboreshwa ikiwa ni maono yake juu ya mageuzi makubwa katika sekta ya Elimu.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi kuelekea uzinduzi huo.
Amesema siku ya kwanza Rais Dkt, Samia akilihutubia Bunge la Jamhuri la Tanzania alitoa tamko juu ya mageuzi makubwa kwenye sekta ya Elimu ambapo wizara ya Elimu ilianza mchakato ya mapitio ya Sera na Mitaala yake.
"Katika mchakato huu wizara ya Elimu iliweza kushirikisha watu na wadau mbalimimbli wa sekta ya elimu wakiwemo walimu, wanafunzi na hata wananchi," amesema Prof. Mkenda.
Aidha amesema, kazi ya kupitia Sera ya Elimu imekamilika inayosema Sera ya Elimu ya mafunzo ya Mwaka 2014 toleo la 2023 na Mitaala yake.
" Mabadiliko haya ya Sera na Mitaala inakwenda kugusa vizazi na vizazi ni niwazi kuwa ni hatua kubwa ya kuboresha elimu yetu nchini na hoja mbalimimbli katika Sera na Mitaala zinaendelea, "Amesema
Pia amesema kufutia mabadiliko hayo tayari maandailizi ya kuwapiga msasa walimu huku ikitoa ajira kwa walimu 4000 la biashara.
Hata hivyo uzinduzi huo wa Sera ya Elimu na Mitaala utafanyika Januari 31 2025 katika ukumbi wa CCM Jakaya Kikwete Dodoma
0 Comments