Header Ads Widget

RAIS SAMIA ACHANGIWA ZAIDI YA MILIONI 2 NJOMBE ZA KUCHUKUA FOMU KUGOMBEA URAIS 2025.

 

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Ikiwa ni wiki moja imepita tangu chama cha mapinduzi CCM kimpitishe Rais Samia kuwa mgombea pekee wa Urais kwa tiketi ya chama hicho na Dr Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea Mwenza kwa nafasi ya Makamu Rais katika uchaguzi mkuu wa 2025  Maelfu ya wafuasi wa chama cha mapinduzi pamoja na Makundi mbalimbali katika jamii wamefanya maandamano kwa kuridhika na uamuzi huo na kisha kuchangishana fedha kiasi cha Mil 2,060,000 zitakazotumika na viongozi hao kuchukua fomu za urais muda utakapofika.

Makundi hayo ni pamoja na Mama Ntilie,Wanamuziki,Viongozi wa Kimila,Dini na Walimu ambapo wamekiri kuridhishwa na utendaji kazi wa viongozi hao huku wakichanga Fedha kwa ajili ya Fomu ya kugombea Urais.

Wakiweka wazi kilicho wasukuma kufanya maandamano ya amani na kisha kuchangishana fedha kwa ajili ya kumlipia fomu ya kugombea Urais wafuasi wa chama cha mapinduzi na wawakilishi wa makundi mbalimbali ambayo yameshiriki katika maandamano hayo akiwemo Chief Wawabena Charles Mkongwa wamesema ni kupongeza na kuunga mkono maamuzi ya chama ya kupitisha majina hayo kwasababu wamekuwa na uongozi bora unaosikiliza na kutatua kero za watanzania zilizowasumbua kwa miaka mingi katika sekta mbalimbali.


Kwa upande wake Julius Peter ambae ni katibu wa CCM mkoa na Deo Sanga Mwenyekiti wameguswa na mwamko mkubwa wa watu katika suala la Mgombea Urais na Mgombea mwenza na kisha kutoa msimamo wa chama mkoa huku mwenyekiti akimpongeza aliyekuwa kiongozi wa chadema kwa kufanya maamuzi ya kujiunga na chama tawala huku akitaka vifaa vya chadema virudhishwe kwenye chama hicho.



Kuhusu maeneo ambayo wangetamani yaguswe katika kipindi cha miaka mitano ijayo mkoani Njombe Wafuasi wa chama tawala wanasema ni Ubovu wa barabara ya Itoni Lusitu na Zile za Mitaani ,maji na Elimu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI