NA HADIJA OMARY
Nibu waziri wa wizara ya maji mhandisi Kundo methew apiga marufuku kwa mamlaka za maji nchini kuwasitishia huduma wateja wa za maji wanaoshindwa kulipia huduma hiyo badala yake amezitaka mamlaka hizo kutafuta njia mbadala ya kuwasaidia ikiwemo kuwafungia mita za malipo ya kabla( pre paid)
Naibu waziri Mhandisi Kundo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kikao kazi kilichowakutanisha wataalamu wa sekta ya maji Mkoani humo ambapo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wajibu wao wa kuwahudumia vizuri wananchi ikiwemo kuwa sehemu ya utatuzi wa changamoto zinazowakabili
Mhandisi kando Amesema anatamani kuona mwananchi mwenyewe anajisitishia huduma kwa kukosa kulipia huduma badala ya mamlaka kwenda kuwakatia maji jambo ambalo utumia rasilimali nyingi kama vile muda na gharama kubwa kwa mteja kuliko wangewafungia Mita za malipo ya kabla
Tunasema kwamba maji ni uhai, Mimi nadhani badala ya kukimbilia kwenye swala la kusitisha huduma ya maji kwa mtanzania , Mimi natamani mtanzania mwenyewe ajikatie maji
Atajikatiaje maji kwa kumfungia prepaid water meter ukishamfungia hiyo huitaji kwenda kumkatia maji yeye mwenyewe atajikatia na Serikali hatutakuwa na lawama yeyote
Hata hivyo akazitaka mamlaka za maji kuandaa mpango maalumu kwa wateja wanaodaiwa kwamba badala ya kuwasitishia huduma basi waweze kulipa kigogo kidogo kwa kulibeba Deni lake kila anapolipa Deni jipya
" Mnawawekea utaratibu mzuri anapokiwa anaendelea kulipia Yale maji yake mapya kuna Ka asilimia mnakubaliana anakuwa analipa huku akiendelea kupata huduma hatuna sababu ya kumkatia maji mtanzania kwa maana unataka apate tabu
Amesema kwa kumkatia mteja huduma ya maji ni wazi kuwa ataenda kutafuta maji ambayo sio salama na hatimae atapata magonjwa ya mlipuko yanayotokana na kukosa maji Safi na hivyo malalamiko yote yatarudi kwa Serikali
Akieleza Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji Katika Mkoa huo Meneja wa wakala wa maji Safi na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) Mhandisi Muhibu Lubasa Amesema kwa sasa kumekuwa na ongezeko la upatikanaji wa huduma ya maji Safi Katika Mkoa huo ambapo umeongezeka kutoka asilimia 53.6 Hadi kufikia asilimia 66.1 kwa upande wa mjini
Amesema huduma hiyo pia kwa upande wa vijijini imeongezeka kutoka asilimia 58 Hadi asilimia 63
Hata hivyo Mhandisi Lubasa Amesema kuwa uwepo wa mitambo ya kuchimbia visima imeweza kutatua changamoto ambapo imekuwa tofauti na hivyokuwa hapo Awali ambapo mamlaka ilikuwa ikichukua muda mrefu kufikisha huduma ya maji endapo kuna sehemu imeonekana kuwa na ukosefu wa huduma hiyo ya maji
0 Comments