Header Ads Widget

DC NJOMBE AUNDA KAMATI MAALUMU KUCHUNGUZA CHANGAMOTO ZA VIWANDA VYA CHAI

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Changamoto ya kutowalipa wakulima na wafanyakazi wa sekta ya chai mkoani Njombe imetajwa kusababisha baadhi ya wakulima kutelekeza mashamba ya chai na kujikita kupanda mazao mengine.


Baadhi ya viwanda hivi sasa vinaonekana kutofanya kazi na vingine kushindwa kuwalipa wakulima na wafanyakazi wao hatua iliyochagiza wakulima kukiona Kilimo Cha chai mwiba mkali.


Migomo ya wafanyakazi kwenye viwanda vya chai mkoani Njombe imekuwa ya mara kwa mara ikisababishwa na kucheleweshewa Mishahara yao na kusababisha serikali kuingia lawamani.



Katika Kikao Cha Ushauri wilaya ya Njombe DCC Baadhi ya wadau wa chai na wakulima wamevitupia lawama viwanda na wawekezaji wa chai huku wakitaka hatua za maksudi Kuchukuliwa ili kunusuru adha kwa wakulima na wafanyakazi.


Baadhi yao ni Mzee Lukule Mponji,Yotham Mhiche,Ally Mhagama na Mchungaji Nelson Godiwe ambao wanasema Tanzania inahujumiwa katika sekta ya chai na kuwakandamiza wakulima na hivyo wawekezaji wababaifu waondolewe mara moja.


Mbunge wa Jimbo la Lupembe  Edwin Swalle amependekeza kuundwa kwa Tume itakayochunguza mkwamo wa viwanda vya Chai Njombe ili kupata suluhu ya Kudumu ili kunusuru sekta hiyo.


Theofhord Ndunguru mkurugenzi mkuu Wakala wa Maendeleo ya wakulima wadogo wa Chai nchini anasema Kuporomoka kwa soko la zao Hilo  duniani kutokana na kushuka kwa unywaji wa chai kuliko uzalishaji Na hivyo kumesababisha  adha kubwa kiuchumi jambo linalosabisha wakulima na wafanyakazi Wengi kulalamika.



Ndunguru  amesema viwanda vingi vya chai duniani vikiwemo vya Kenya Uganda na Tanzania vimefungwa kutokana na hasara kubwa ya uendeshaji.


Naye Jaherson Moturi ni mkurugenzi wa viwanda vya Chai vya Kampuni ya DL Group ambaye amekiri kuchelewesha malipo ya wafanyakazi na kwa kiwanda Cha kibena wanadaiwa Mishahara ya Mwezi Mmoja Ambayo Wanatarajia kuilipa hivi karibuni na Ikanga Lupembe miezi miwili.



Kutokana na changamoto hizo mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amelazimika kuunda Kamati maalumu ya uchunguzi itakayofanya kazi ya kufuatilia changamoto za viwanda vya chai ili ije na majibu sahihi yatakayowasaidia wakulima na wafanyakazi kupata Fedha zao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI