Header Ads Widget

MANGA FC YATWAA KOMBE LA JOLLAM PROPERTY CUP NJOMBE

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Timu ya Soka ya Manga kutoka Kijiji Cha Manga kilichopo kata ya Madilu wilaya ya Ludewa mkoani Njombe imefanikiwa kutwaa kombe la JOLLAM PROPERTY CUP Baada ya kumchakaza Mfalasi FC kwa bao Moja kwa Nunge katika mashindano yaliyoshirikisha Timu sita za vijiji vya kata hiyo.


Akikabidhi kombe Hilo,Fedha kiasi Cha shilingi laki Tano pamoja na Medali Mgeni wa Heshima Olivanus Thomas Mkuu wa wilaya ya Ludewa amewataka vijana kuepukana na makundi hatarishi kwa kushiriki katika michezo pamoja na kuhakikisha wanashiriki vyema katika zoezi la uhuishaji taarifa katika Daftari la kudumu la mpiga kura ili waweze kupata fursa ya kushiriki uchaguzi mkuu Mwaka huu.



Awali Mkurugenzi wa Kampuni ya JOLLAM PROPERTY CO.LTD Josaya Luoga amesema mashindano hayo yaliyoandaliwa na Kampuni hiyo inayojihusisha na masuala ya upimaji Ardhi yalilenga kuhamasisha wananchi kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa hapo Mwaka jana na kuliendea zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la mpiga kura katika uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.


Aidha Luoga  amesema awamu ijayo watapanua Wigo na kupeleka Ligi hiyo kwenye kata nyingine ili vijana wapate fursa zinazotokana na michezo na kuiweka miili yao sawa.



Naye mkurugenzi mwenza wa Kampuni hiyo Bwana Lawi Mnyange amesema Ligi hiyo itakuwa ikifanyika kila Mwaka  ili vijana waachane kabisa na starehe zinazoweza kuwasababishia madhara kiafya kwa kutojihusisha na michezo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI