Na. Mwandishi Wetu, Kigamboni.
KLABU ya mchezo wa Jogging ya mbio fupi fupi katika kuimarisha Afya, inayofahamika kama 'Maendeleo Mbwamaji Jogging Sports Club' imezinduliwa rasmi tarehe 25 Januari 2025, kwa lengo la kuwakusanya Vijana pamoja kufanya mazoezi na kupata elimu ya Ujasiriamali.
Awali akitoa taarifa juu ya kikundi hicho, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbwamaji, Mhe. Yohana Luhemeja 'Maziku' amesema alipata wazo la kuwakusanya vijina pamoja ilikujenga miili yao katika Afya pamoja na kuwapa elimu ya Ujasiriamali.
"Kikundi hiki kipo chini ya usimamizi wa Serikali ya Mtaa wetu wa Mbwamaji. Hadi sasa kina Wanachama 45, wakiwemo Wanawake 30 na Wanaume 15.
Hadi sasa wamepatiwa mafunzo ya utengenezaji wa sabuni za maji na sabuni za vipande, Ushonaji nguo na utengenezaji wa batiki, hata hivyo changamoto kubwa inayokabiri ni ukosefu wa vitendea kazi kama mashine za kutengenezea sabuni ambazo ni Tsh 17,000,000." Amesema Yohana Luhemeja Maziku.
Kwa upande wake Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Katibu Kata wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Juma Luja amepongeza Klabu hiyo ya Jogging na kuweza kuchangia Tsh.200,000 na akaahidi kushirikiana na Mwenyekiti wa Mtaa ndg Yohana Luhemeja Maziku kuendelea kusaidia kikundi kwa kutafuta wadau wa kusaidia upatikanaji wa mashine hizo.
Nae Mwenyekiti wa kikundi hicho, Bi.Tatu Sungu amemshukuru Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbwamaji kwa kuwasaidia kwa hari na mali muda wote wanapo hitaji msaada.
Nae Katibu wa ccm tawi la Gezaulole, Abdallah Ntandu ambye ameweza kushiriki mazoezi na vijana wa kikindi hicho amesema:
"Mazoezi ni afya, kwahiyo tujitahidi kutenga muda kwa ajili ya kufanya mazoezi kwa kuimarisha miili yetu" amesema.
Katika tukio hilo, wadau mbalimbali wameweza kujitokeza kwa wingi kushiriki ambapo pia kulikuwa na ukataji wa keki.
0 Comments