Header Ads Widget

HESHIMA KUBWA TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA NISHATI AFRIKA- AIDAN MLAWA

 

Na Matukio Daima media 

Tanzania inajivunia nafasi ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu Nishati (Africa Energy Summit) unaofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 27-28 Februari 2025, chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Mdau wa maendeleo wilayani Kilolo mkoani Iringa Aidan Mlawa akizungumza na Matukio Daima Tv leo amesema kuwa hii ni heshima kubwa kwa taifa, ikionyesha mchango na juhudi za Tanzania katika kusimamia na kuendeleza sekta ya nishati barani Afrika.

 Mlawa anasema  kuwa mkutano huu ni fursa adhimu kwa Tanzania kuimarisha mahusiano ya kiuchumi, kufungua milango kwa uwekezaji mpya, na kuimarisha nafasi yake katika ramani ya maendeleo ya nishati barani Afrika. 

Kuwa Sekta ya nishati ni msingi wa maendeleo ya kiuchumi, na mkutano huu unatoa fursa ya kubadilishana mawazo, teknolojia, na kushirikiana katika miradi ya kimkakati ya nishati.

Anasema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika sekta ya nishati, hasa kupitia uwekezaji wa miradi mikubwa inayolenga kuzalisha na kusambaza umeme kwa gharama nafuu. 

Kuwa kwa mujibu wa takwimu za serikali, zaidi ya asilimia 78 ya nishati ya umeme nchini inatokana na vyanzo safi kama maji, gesi asilia, na jua. 

"Hii ni hatua muhimu kuelekea uchumi endelevu na unaozingatia mazingira hata  hivyo, bado kuna changamoto, hususan katika maeneo ya vijijini ambako asilimia kubwa ya wananchi hawajafikiwa na huduma ya umeme"

Anasema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, imeweka mikakati kabambe ya kuhakikisha nishati inapatikana kwa wote ifikapo mwaka 2030, sambamba na malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs).

Mlawa anasema serikali ya Tanzania imeweka juhudi kubwa katika kuboresha miundombinu ya nishati kupitia miradi mbalimbali.


Kwani Mradi wa Bwawa la Nyerere (JNHPP) kuwa Bwawa hili linajengwa katika Mto Rufiji na linatarajiwa kuzalisha megawati 2,115 za umeme.

Hivyo  Mradi huu unalenga kuboresha upatikanaji wa umeme wa uhakika na wa gharama nafuu kwa wananchi na viwanda.

Pia  Mradi wa Kiwanda cha Gesi Kinyerezi I na II kuwa Gesi asilia ni moja ya rasilimali kuu za nishati nchini. 

Pia alisema Kiwanda cha Kinyerezi kinazalisha jumla ya megawati 336, na upanuzi wa miradi mingine unaendelea ili kuongeza uzalishaji wa umeme 

Mlawa anasema kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), serikali imefanikiwa kupeleka umeme kwa zaidi ya vijiji 10,000. 

"Mpango huu umeboresha maisha ya wananchi, kuongeza fursa za kiuchumi, na kuboresha utoaji wa huduma za jamii kama vile afya na elimu"

Anasema kuwa Tanzania pia inawekeza katika nishati jadidifu kama vile umeme wa jua na upepo. 

Hivyo Mradi wa upepo wa Singida na miradi ya jua mikoa ya Dodoma na Shinyanga ni hatua kubwa katika kuboresha mchanganyiko wa nishati nchini.

Mlawa anasema kuwa mkutano huu wa Nishati Afrika unaleta faida nyingi kwa Tanzania, zikiwemo kama kuvutia Uwekezaji kuwa Kupitia mkutano huu, Tanzania itapata nafasi ya kuwakaribisha wawekezaji wa kimataifa wenye nia ya kuwekeza katika sekta ya nishati, viwanda, na miundombinu.

"Mkutano huu ni jukwaa la kujifunza teknolojia mpya zinazoweza kuboresha uzalishaji na usambazaji wa umeme, hasa katika maeneo yasiyofikiwa na gridi kuu"anasema Mlawa

Kuwa Tanzania itaimarisha ushirikiano wake na nchi jirani kupitia miradi ya pamoja kama bomba la mafuta la Afrika Mashariki (EACOP) na gridi za umeme za kikanda.


Pamoja na fursa hizo pia Kuongezeka kwa uwekezaji kutaleta ajira kwa Watanzania katika sekta za ujenzi, uzalishaji, na usimamizi wa miradi ya nishati.

Anasema kuwa Miradi ya nishati inatoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi kupitia mapato ya kodi, upatikanaji wa umeme wa uhakika, na kuchochea maendeleo ya viwanda.

Serikali ya Tanzania imeweka msukumo mkubwa kuhakikisha upatikanaji wa umeme kwa kila Mtanzania:

Kuwa mpango huu umewezesha kuunganisha vijiji 12,000 na gridi ya taifa, na serikali inalenga kuongeza asilimia ya upatikanaji wa umeme vijijini kutoka asilimia 60 hadi 75 ifikapo mwaka 2026.

Hivyo Serikali imeboresha miundombinu ya usambazaji wa umeme, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa njia za kusafirisha umeme zenye msongo mkubwa kutoka maeneo ya uzalishaji kwenda kwa walaji.

Anasema kuwa Tanzania inatekeleza miradi ya nishati jadidifu kama vile upepo, jua, na biogesi, ambayo ni suluhisho endelevu kwa changamoto ya ukosefu wa umeme maeneo ya mbali.


Mlawa ambae pia ni kada wa CCM anasema kuwa heshima ya Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Nishati Afrika ni ushahidi wa juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuboresha sekta ya nishati ni kubwa .

Hivyo  Miradi mikubwa ya umeme kama Bwawa la Nyerere, Kinyerezi, na REA imeonyesha dhamira ya serikali katika kufanikisha maendeleo ya kiuchumi kupitia upatikanaji wa nishati.

Mlawa anasema kuwa mkutano huu unaleta fursa nyingi za kiuchumi, kijamii, na kimazingira, na ni ishara ya msimamo wa Tanzania kama kiongozi wa maendeleo ya nishati barani Afrika

Hivyo ni wakati muafaka kwa Watanzania wote kushirikiana katika kufanikisha malengo haya kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vijavyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI