Header Ads Widget

YOHANA LUHEMEJA AANZA KAZI KWA KISHINDO, ATINGA DAWASA, AKAGUA MIUNDOMBINU YA MTAA WA MBWAMAJI

 


Na.Matukio Daima App, Kigamboni.

 

MWENYEKITI wa  Serikali ya Mtaa wa Mbwamaji uliopo Gezaulole Kata ya Somangila Manisapaa ya Kigamboni, Mhe. Yohana Luhemeja 'Maziku' kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameendelea na ziara maalum katika kufuatilia kero pamoja na kukagua miradi yenye changamoto ikiwemo upatikanaji wa maji safi, huduma ya Afya na miundombinu katika mtaa huo wenye historia kongwe hapa nchini.


Awali Mhe. Maziku ameweza kukutana na Wajumbe wote pamoja na kamati ya Mtaa katika kikao maalum kujitambulisha pamoja na kupokea maoni na ushauri ndani ya mtaa huo ambapo kisha ameweza kukagua miundombinu ya barabara zote za mtaa zenye changamoto.


Aidha, ameweza kutembelea ofisi za Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) Gezaulole zilizopo mtaa huo wa Mbwamaji.


Akiwa Dawasa ameweza kupokea ripoti za upatikanaji wa maji safi sambamba na miundombinu ya mabomba ambayo yameshatandazwa ardhini katika baadhi ya maeneo ya mtaa huo.


Awali, Injinia wa Dawasa, Aron Musa amebainisha kuwa, Mtaa huo unapata maji kwa asilimia kubwa bila changamoto licha ya Wananchi wengi kushindwa kuomba kuunganishiwa Huduma hiyo.


"Hadi sasa wateja zaidi ya 60 tayari wameunganishiwa maji ya DAWASA kutokea hapa kwenye mtambo wetu wa Mbwamaji.


Lakini pia miundombinu ya mabomba imesambazwa na tunaunganisha  kwa wateja wote wenye uhitaji," Amesema Injinia Aron Musa -Dawasa Mbwamaji.


Kwa upande wake, Mwenyekiti Mhe. Maziku ameishukuru Dawasa kwa hatua hiyo huku akiwaomba kuongeza kasi uwekaji wa miundombinu ya mabomba eneo la katikati ya makazi ya mtaa huo ambao bado maji hayajafika na uhitaji ni mkubwa.


"Lengo la kufika hapa ni kuhakikisha Wananchi wanapata huduma iliyo sahihi, Tuhakikishe tunafanya kazi zetu za Wananchi kupata Huduma bora.


"Niwashukuru sana, Kisima hiki kilikuwa kimekufa kabisa kwa muda mrefu. Nilipoingia 2010 nilipokuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa hapa kwa mara ya kwanza nilipambana na kuweza kukifukua na kufanya kazi 


Lengo kubwa mifumo ya maji iendelee kuwekwa na Wananchi waunganishiwe maji hata ikiwezekana kwa mkopo iliwakatwe kidogokidogo kwenye bili zao." Amesema Mhe Maziku.

Aidha, Mhe Maziku pia ameweza kukagua baadhi ya Miundombinu ya barabara ya Mtaa huo wa Mbwamaji na kushuhudia ubovu na uchakavu ambapo ameahidi kwa kushirikiana n Manisapaa ya Kigamboni pamoja na Wadau watatatua kero zilizoonekana ilikusaidia Wananchi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI