Wajasiriamali wanaofanya biashara pembezoni mwa Msikiti wa Mtoro wameiangukia Serikali kuingilia kati mgogoro unaoendelea kati yao na uongozi wa msikiti huo ambapo umewataka Wafanyabiashara kuondoka eneo la barabara ambalo wanafanyia biashara kabla na baada ya matengenezo ya barabara.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa Wafanyabiashara hao Simba Lichanda amesema eneo hilo ndilo wanategemea kufanya biashara ili kutunza familia zao na wapo hapo kwa muda mrefu na viongozi wengi wanasuali na hakukuwahi kuwa na tofauti yeyote walipohitajika kupisha kwaajili ya shughuli mbalimbali za msikiti huo walifanya hivo.
Wamuomba Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aingilie kati wasiondolewe eneo hilo na kwamba wapo tayari kufuata maelekezo watakayopewa na serikali ilimladi tu waendelee na shughuli za eneo hilo ambalo tayari Wana umoja wao uliosajiliwa serikalini.
Amesema ujumbe waliopokea unawataka kuendelea kuondoka katika maeneo hayo haraka hadi kufikia jumatatu 23 Desemba 2024 wataondolewa kwa nguvu.
0 Comments