Wafungwa 6,000 wameripotiwa kutoroka katika Gereza Kuu la Maputo Siku ya Krismasi (Desemba 25, 2024) huku Wafungwa 33 wakiuawa na wengine 15 kujeruhiwa wakati wa makabiliano kati ya Wafungwa na Vikosi vya Usalama
Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi, miongoni mwa Wafungwa waliotoroka wapo Magaidi 29, kitendo kinachoongeza wasiwasi juu ya Usalama wa Taifa hilo huku Vurugu za kupinga Matokeo ya Uchaguzi Mkuu zikiendelea
Kutoroka kwa Wafungwa kulitokea wakati wa Maandamano yenye vurugu yaliyochochewa na Baraza la Katiba kuthibitisha ushindi wa Chama Tawala cha FRELIMO katika uchaguzi wa Oktoba 9. Maandamano hayo yameripotiwa kusababisha uharibifu mkubwa wa Miundombinu, Magari na Vituo vya Polisi.
0 Comments