Header Ads Widget

WADAU RUKWA WATAKIWA KUWA MABALOZI UHAMASISHAJI WANANCHI KUJIANDIKISHA NA KUBORESHA TAARIFA ZAO DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA


 Na Matukio Daima App, Rukwa.

Martin Mnyenyelwa kaimu Mkurugenzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi amesema kuwa tume inatarajia kupata ushirikiano mkubwa zaidi kutoka kwa wadau mbalimbali walioshiriki kwa kuwafikishia Wananchi wa Mkoa wa Rukwa taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa kuwahamasisha wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha.


Ameyasema hayo katika mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi mkoani Rukwa katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Sumbawanga  uliohudhuriwa na Wadau mbalimbali ikiwemo viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, wawakilishi wa asasi za kiraia, wahariri wa vyombo vya habari, waandishi wa habari, maafisa habari wa mikoa na halmashauri, wawakilishi wa makundi mbalimbali ya vijana, watu wenye ulemavu, wanawake na wazee wa kimila.


"Ni matarajio ya Tume kuwa mtakua mabalozi wazuri wa kusambaza taarifa na kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao ili zoezi hilo lifanyike kwa ufanisi na kwa matokeo makubwa". alisema Mnyenyelwa 


Mnyenyelwa Ameongeza kuwa lengo la mkutano huo ni kuwapa taarifa za uwepo wa zoezi hilo ambalo litafanyika kwa siku 7 kuanzia tarehe 12/01/2025 hadi 18/01/2025 na kuwapitisha katika mifumo ya uandikishaji pamoja na kuona namna zoezi litakavyofanyika vituoni na taarifa za maandalizi ambayo yanajumuisha uhakiki wa vituo vya wapiga kura, uboreshaji wa majaribio, ununuzi wa vifaa na ushirikishwaji wa wadau.


Hata hivyo amewaomba viongozi wa vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi kuzingatia sheria ya uchaguzi, kanuni za uboreshaji, maelekezo ya tume na kusimamia miiko na mipaka ya uendeshaji wa zoezi la uboreshaji wa daftari huku akisisitiza kuwa mawakala au viongozi wa vyama vya siasa hawaruhusiwi kuingilia mchakato wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kituoni.


Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi NEC, Kwa kuzingatia  mashariti  ya kifungu cha 9(1) na (2) cha sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na ya Mwaka 2024 pamoja na vifungu vingine  vinavyohusu uandikishaji  na Uboreshaji, zoezi hilo lina husisha mambo muhimu ambayo ni;-


Kuandikisha Wapiga Kura wapya  amabo ni Raia wa Tanzania  wenye umri wa miaka 18 na zaidi na watakao timiza  umri huo  ifikapo tarehe ya Uchaguzi Mwaka 2024.


Kutoa fursa Kwa Wapiga Kura waliopo kwenye Daftari na ambao wamehama, ili waweze kuhamisha  taarifa zao kutoka  kata au Jimbo walilonandikiashwa awali.

 Kutoa fursa Kwa Wapiga Kura walilonandikiashwa kurekebisha taarifa zao yakiwemo majina  na taarifa nyingine.


 Kutoa kadi mpya  Kwa Wapiga Kura Walipoteza kadi  au kurekebisha kadi zao zilizo haribika


Kuondoa taarifa ya  Wapiga Kura Walipoteza sifa za kuwepo kwenye Daftari la  kutokana na sababu mbalimbali  ikiwa ni pamoja na kuukana uraia wao wa Tanzania au kifo.


Kaulimbiu ya uboreshaji wa daftari la kudumu la yawapiga kura 2024/2025 inasema "KUJIANDIKISHA KUWA MPIGA KURA NI MSINGI WA UCHAGUZI BORA".




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI