NA AMINA SAIDI,Matukio Daima media TANGA.
Waandishi wa Habari Mikoa mbalimbali nchini Tanzania wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo katika kuandika habari juu ya masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na Shirika lisilo la kiserikali CAN Tanzania lililopo jijini Dar esalaam
Wakizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mkutano wa ofisi za CAN wamelipongeza Shirika hilo kwa mafunzo hayo kuwa yatawasaidia kuimarisha utendaji Kazi katika kuripoti habari za mabadiliko ya tabia nchi kwa uweredi zaidi.
Pamoja na mafunzo hayo yaliyotolewa kuwajengea uwezo kitaaluma wamesema wataongeza bidii katika kuripoti habari zenye kuakisi maisha halisi ya jamii ili kujenga uwelewa wa maana halisi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Mafunzohayo yaliyoanza tarehe 2 Disemba na kuisha Disemba 4mwaka huuu yamewashirikisha Waandishi wa Habari kutoka Mkoa wa Dar esalaam,Morogoro,Arusha,Tanga pamoja na Zanzibar kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuandika habari za mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa upande wake mkurugenzi WA Shirika la CAN Tanzania Dr Sixbert Mwanga amesema kuwa Waandishi wa Habari wanatakiwa kutumia kalamu zao kuandika makala na vipindi mbalimbali vinavyohusu masuala ya mabadiliko ya tabia nchi.
"Pia anatoka wito kwa wahariri kuhakikisha mabadiliko ya tabia nchi yanapewa kipaumbele kwenye kurasa na vyombo vya habari ni muhimu Sana itakuwa tumetoa mchango mkubwa Sana "alifafanua Dr Mwanga.
Kupitia mafunzo hayo yaliyotolewa kwa siku tatu Waandishi wa Habari wamesema yamewawezesha kugundua fursa ndani ya changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi nchini.
0 Comments