Na Matukio Daima Media, Dar es Salaam
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nidhati na Maji (EWURA) imewataka Watanzania kuwatumia mafundi umeme wenye leseni za EWURA kufunga mfumo wa umeme ndani ya nyumba ili kuepukana na majanga ya moto yanayotokana na hitilafu za umeme.
Rai hiyo imetolewa leo Desemba 13, 2024 jijini Dar es Salaam na Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano, Titus Kaguo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dk. James Andilile katika Mafunzo ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji kwa Chama Cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA).
Kaguo amewataka Wanachama wa JOWUTA kuandika Habari za kuhamasisha Watanzania kuwatumia mafundi wenye leseni za EWURA ili kupunguza majanga ya moto yanayotokana na hitilafu ya ufungaji usio salama wa nyaya za umeme katika nyumba za wananchi."Katika kipindi cha Miaka mitatu tumetoa leseni 8,000 kwa mafundi umeme wa nyumba za makazi ya wananchi, tuwatumie mafundi hao kwa sababu leseni yetu inawapa kibali cha kufanyakazi popote nchini" amesema Kaguo.
0 Comments