Header Ads Widget

NJEZA AMLILIA BABA WA MWENEZI CCM WILAYA YA MBEYA



Mheshimiwa mbunge wa jimbo la Mbeya vijijini mkoani Mbeya Oran Njeza, ameshiriki ibada ya mazishi ya Yoramu Jilla ambaye ni baba mzazi wa katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Mbeya vijijini Lameck Jilla aliyefariki Dunia Desemba 11, 2024.


Katika msiba huo, Mhe. Njeza amewashukuru wananchi kwa kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa amani na utulivu.


Marehemu Yoramu Jilla amezikwa katika makaburi ya familia katika kijiji na kata ya Isuto Tarafa ya Isangati Mbeya vijijini, msiba uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi na Serikali.


Mbunge wa Mbeya vijijini Mhe. Oran Manasse Njeza, amewataka wananchi kuendelea kuishi kwa kuweka imani na tumaini lao kwa Mungu huku wakifanya kazi kama ambavyo imekuwa msisitizo wa Serikali ya awamu ya sita na kauli mbiu yake ya kazi iendelee.


Mbunge Njeza amewapongeza na kuwashukuru wananchi kufanikisha kuchagua viongozi wanaowataka kwenye uchaguzi uliopita wa Serikali za mitaa kwa amani na utulivu na kuendelea kuhimiza wananchi kutunza amani iliyopo ili kuchochea maendeleo.



Naye mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mbeya vijijini Akimu Sebastian Mwalupindi, pamoja na kutoa salamu zake za rambirambi kwa familia ya Jilla, ameeleza kuwa familia hiyo imekuwa baraka kwa kutoa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ambayo ni kwa ajili ya kuisimamia Serikali.


"Ndugu zangu marehemu mzee Jilla alikuwa kiongozi alikuwa mwenezi wa tawi, mtoto wake Lameck Jilla ni katibu mwenezi Wilaya ya Mbeya vijijini halafu mjukuu wake (Yusuph Lameck Jilla) ni katibu mwenezi wa CCM kata ya Isuto kwahiyo mtaona jinsi ambavyo mzee Yoramu Jilla ametuachia zawadi ya viongozi na mnaona maendeleo yanayoendelea kuletwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ambayo tunaisimamia", amesema Mwalupindi.


Aidha kiongozi huyo amewashukuru wananchi katika wilaya ya Mbeya vijijini na mkoa wa Mbeya kwa ujumla kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa amani na utulivu na kuwaasa kuendelea kulinda umoja na mshkamano uliopo nchini.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI