Na Lilian Kasenene,Morogoro
Matukio DaimaApp
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Eng. Mwajuma Waziri amemtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa Bwawa la Kidunda Sinohydro kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi huo na kuukamilisha kwa wakati ili kufikia malengo ya serikali.
Eng. Mwajuma aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Bwawa hilo linalotarajia kuhifadhi kiasi cha maji mita za ujazo Milioni 190 pindi litakapo kamilika.
Alisema nia ya Serikali ni kuhakikisha bwawa hilo linamaliza changamoto ya huduma ya maji katika mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es salaam.
Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Maji alisema utekelezaji unaenda vyema na juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan zinaonekana, kwani fedha tayari zipo.
"Ni muda sasa wa mkandarasi wa huu mradi kufanya kazi kwa bidii ili wananchi wanufaike na hili Bwawa la Kidunda,"alisema.
Katika ziara hiyo Eng. Mwajuma aliambatana na Kamishina wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha Meshack Anyingisye ambaye alikiri kufurahishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa Bwawa hilo,huku akiiomba Wizara ya Maji kuendelea kuweka uangalizi wa kutosha ili mradi uweze kukamilika kwa wakati kama ilivyokusudiwa










0 Comments