Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Tume huru ya uchaguzi imewaonya wale watakaothubutu kujiandikisha zaidi ya mara moja kwenye Daftari la kudumu la mpiga kura kupitia zoezi linalotarajia kuanza hapo Januari 2025 mkoani Njombe kwani kufanya hivyo ni kinyume Cha Sheria.
Onyo Hilo limetolewa na Mtibora Selemani mkurugenzi wa kitengo Cha huduma za Sheria Tume huru ya Taifa ya uchaguzi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume hiyo katika mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoani Njombe ukilenga kuliendea zoezi la uboreshaji wa daftari la mpiga kura na kwamba kujiandikisha zaidi ya mara moja ni kukiuka Sheria za uchaguzi.
Aidha amesema Jumla ya Mikoa 21 imekamilisha zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura huku mkoa wa Njombe ukitarajia kuendesha zoezi Hilo kuanzia Januari 12 Hadi 18 Mwaka 2025 yakiwa ni Maandalizi ya uchaguzi mkuu Ujao.
Akitoa mada Katika mkutano huo Stephen Elisante Mkurugenzi msaidizi Idara ya usimamizi wa Uchaguzi amesema Katika mkoa wa Njombe Jumla ya wananchi 80994 wanatarajiwa kujiandikisha katika Daftari la kudumu la mpiga kura na kwamba vijana wanapaswa kuwahamasisha wenzao kwa wingi na kujiepusha na upotoshwaji.
Wadau wa Uchaguzi wakiwemo viongozi wa Vyama vya Siasa na Viongozi wa Dini mkoani Njombe wamesisitiza haki katika mchakato huo hadi uchaguzi hapo 2025.
Lewis Mnyambwa ni mratibu wa uandikishaji mkoa wa Njombe ambaye anasema zoezi la utoaji mafunzo kwa waandikishaji wasaidizi linaanza kesho katika ngazi mbalimbali.
0 Comments