Na. Mwandishi Wetu, Kigamboni.
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa wa Mbwamaji uliopo Gezaulole Kata ya Somangila Wilayani Kigamboni Mhe. Yohana Luhemeja 'Maziku' kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameendelea na ziara maalum katika kufuatilia kerop, amoja na kukagua miradi yenye changamoto ikiwemo upatikanaji wa maji safi, huduma ya Afya na miundombinu katika mtaa huo wenye historia kongwe hapa nchini.
Akiwa Zahanati ya Gezaulole ameshuhudia uchakavu wa majengo ikiwemo kuvuja ambapo ameahidi kushirikiana na Manisapaa ya Kigamboni na Wadau ilikuweka mazingira rafiki ya huduma katika Zahanati hiyo.
"Nimekuja kutembelea Zahanati yetu ya Gezaulole iliyopo hapa Mtaa wa Mbwamaji.
Nimeona mifumo ya maji safi na maji taka imeziba, lakini pia miundombinu ya barabara za mtaa ni mbovu zote.
Suala la Wafanyakazi hawapati malipo yao kwa muda mfano, Mlinzi na wafanya Usafi, Uongozi ulishatoa taarifa Manisapaa, Naomba niwaahidi kama Mwenyekiti wa Mbwamaji, nitalipatia utatuzi ikiwemo kumwandikia tena barua Mkurugenzi wa Kigamboni kutatua changamoto.
Lakini pia Uongozi wa Mtaa wa Mbwamaji utatafuta wadau kusaidia kutatua changamoto hizi" amesema Mhe Yohana Luhemeja 'Maziku'.
Aidha, amewatia moyo watendaji wa Zahanati hiyo kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma kwa moyo wote kama wito na viapo vyao katika kusaidia Jamii ya Watanzania.
Zahanati hiyo ni moja ya Zahanati Kongwe katika Mtaa huo wa Mbwamaji Mtaa ambao upo katika historia za Nchi ikiwemo mji wa Pwani wa kale.
0 Comments