Header Ads Widget

THRDC YASISITIZA UMUHIMU WA KUIMARISHA MAKUNDI YA KIJAMII KATIKA UTETEZI WA HAKI ZA BINADAMU

                   ONESMO OLE NGURUMWA, MRATIBU WA THRDC
Na Matukio Daima media 

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa, ameelezea umuhimu wa kuimarisha makundi ya kijamii yanayotetea na kulinda haki za binadamu hapa nchini.

Amesema kuwa juhudi hizo zitasaidia kila mwanajamii kutimiza jukumu lake la kuilinda na kuhifadhi haki hizo za msingi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa wadau wa haki za binadamu na wanahabari, Ole Ngurumwa amesema kuwa mkutano huu umeandaliwa, kuadhimisha Siku ya Haki za Binadamu Duniani, ambayo hufanyika kila mwaka mnamo Desemba 10.

Akifafanua maudhui ya mkutano huo, Ole Ngurumwa amesema ushiriki wa asas za kiraia, wadau wa haki za binadamu pamoja na wanahabari kutaisaidia kijamii kupata uelewa wa haki za binadamu na kutokomeza matukio yanayokiuka haki hizo.

"Kwa kushirikiana kwa pamoja kupitia mazungumzo, tunaweza kuondoa changamoto zinazohusiana na ukiukwaji wa haki za binadamu," alisema Ole Ngurumwa.


                  JENERALI ULIMWENGU MWANAHABARI NGULI NCHINI   

Kwa upande wake, Jenerali Ulimwengu, ambaye ni mwandishi na mchambuzi maarufu wa masuala ya kijamii na haki za binadamu, amesema vyombo vya habari vina umuhimu mkubwa katika ulinzi wa haki za binadamu, hivyo kutoa wito kwa wanahabari kutumia taaluma yao kwa usahihi na kwa kutimiza wajibu wao wa kitaaluma katika kuhabarisha jamii.

Amesema kuwa wanahabari wana jukumu la kuhakikisha wanatetea haki za msingi za kila Mtanzania kupitia habari zao.

Ulimwengu pia, amesisitiza umuhimu wa kupitia upya baadhi ya sheria ambazo zinaweza kuathiri uhuru wa upatikanaji na utoaji wa habari katika mazingira ya uhuru.

               ALIYEWAHI KUWA MTENDAJI MKUU WA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU  HELLEN KIJO BISIMBA

Kwa upande wake, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Hellen Kijobisimba, amesema kuwa ushirikiano wa karibu kati ya asasi za kiraia na vyombo vya habari unahitajika kwa ajili ya kufikisha elimu ya haki za binadamu kwa jamii.


Amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya vyombo vya habari, asasi za kiraia na jamii, kutarejesha matumaini ya kujenga jamii yenye usawa, haki, na maendeleo endelevu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI