Header Ads Widget

PROF. KABUDI MGENI RASMI KONGAMANO LA KIMATAIFA LA AFRIKA YA KESHO




Na. Matukio Daima App, Morogoro 

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Prof Paramagamba Kabudi anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi kwenye Kongamano la kimataifa la Afrika ya Kesho litakalofanyika kwa siku mbili, Desemba 17 na 18,2024 Katika chuo Kikuu cha Jordan JUCO mjini Morogoro ambapo watu zaidi ya 200 watahudhuria.


Kongamano hilo limeandaliwa na taasisi mbalimbali za elimu ya juu vikiwemo vyuo vikuu vya Ndani na nje ya nchi likilenga pamoja na mambo.mengine kuangalia changamoto ya mmomonyoko wa maadili kwenye Utamaduni wa kiafrika unaoletwa na utandawazi.


Kongamano hilo limeandaliwa na chuo Kikuu cha Jordan kwa kushirikiana na chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, Chuo Kikuu cha Waislam MUM na chuo Kikuu cha SUMAIT cha Zanzibar.


Wengine ni chuo Kikuu cha IMO State cha nchini Nigeria, Chuo Kikuu cha Zimbabwe, Taasisi ya Arizona ya nchini Marekani na Portable Practical Educational Preparation (PPEP).


Akizungumza na Matukio Daima mjini Morogoro, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi  Mhadhiri Mwandamizi kutoka chuo Kikuu cha Mzumbe Dkt.Adolph Makauki alisema Kongamano hilo litabeba mambo mbalimbali yanayohusu Siasa, Historia, Uchumi,Maadili, Haki, Urithi, Uhuru pamoja na Lugha.


Akasema mada kubwa Katika kongamano hilo ambako zaidi ya watu 200 nusu yao wakitegemewa kuwa vijana, litakuwa na mada kuu itakayoliongoza inayosema Jitihada za jamii juu ya uhifadhi wa Tamaduni na Lugha za kiafrika.


Naye Mratibu wa kitengo cha Maendeleo ya jamii kutoka chuo Kikuu cha Jordan, Bw.Carol Mattunda aisema maandalizi yote tayari yamekamilika na wanategemea litaleta matokeo chanya Katika kurejesha Tamaduni za kiafrika Katika bara la Afrika hasa kwenye masuala ya maadili kwa vijana.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI