Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa ameishukuru benki ya NMB kwa kutoa vifaa vya kujifungulia mama wajawazito 300 na mashuka 300 kwenye hospitali ya wilaya ya Rufiji.
Mchengerwa alitoa pongezi hizo kwenye hospitali hiyo ya wilaya Rufiji Utete kwa kutoa msaada huo ambao utawasaidia akinamama wakati wa kujifungua.
Mchengerwa amesema kuwa benki hiyo imemuenzi mpigania uhuru Bibi Titi Mohamed ambaye pia ni Mbunge wa kwanza wa Rufiji na imeonyesha uzalendo kwa kuwasaidia wakinamama wajawazito kwenye hospitali hiyo ya Wilaya ya Utete.
"Mmemuenzi Bibi Titi ambaye ni mama pia Rais Dk Samia Suluhu Hassan naye ni mama anayepigania wanawake na wananchi wote wa Tanzania hili ni jambo kubwa sana,"amesema Mchengerwa.
Naye Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam na Pwani Seka Urio amesema kuwa wanaunga mkono jitihada za Serikali kwa kurudisha kwa jamii kwa kukabili changamoto za afya ambapo vifaa hivyo na mashuka vinathamani ya shilingi milioni 12.3.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Michael Mkumbwa amesema kuwa vifaa hivyo vitawasaidia sana akinamama watakapofikia muda wa kujifungua kwani baadhi wamekuwa wakifika bila vifaa.
0 Comments