Header Ads Widget

MDUDE AACHIWA KWA DHAMANA, WAKILI SHITAMBALA AKEMEA POLISI KUKIUKA SHERIA.

Hatimaye Mdude Nyagali Mpaluka ambaye ni mwanaharakati na mwanachama wa CHADEMA, ameachiwa kwa dhamana na mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Songwe baada ya kushikiliwa na jeshi la Polisi tangu Novemba 22 mwaka huu 2024 mkoani Songwe.

Sheria inaelekeza wazi kwamba mtuhumiwa ana haki ya kudhaniniwa ndani ya muda usiozidi saa 24 kwa kosa linalodhaminika tofauti na ambavyo imekuwa kwa mwanaharakati huyo wa haki za binadamu.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukaamilika kwa taratibu za dhamana, wakili Sambwe Shitambala, amelaani kitendo cha Polisi kumshikilia Mdude Nyagali kwa muda wote kuanzia Novemba 22, 2024 hadi Desemba 06, 2024 bila kumpatia dhamana juu ya tuhuma wanazomtuhumu.

"Ndugu yetu Mdude Nyagali bahati nzuri amesomewa mashtaka yake leo (Desemba 06, 2024) na amedhaminiwa kwa sasa, haki ya dhamana ni ya kila mwananchi ambayo kimsingi inatakiwa itolewe mapema iwezekanavyo lakini imechelewa na hili kama mawakili, kama wa-Tanzania tunalaani, hatupendi kuona mwananchi ambaye analindwa na katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania hana haki na uhuru anaostahili wakati sheria inampa haki ya kuwa huru kwa mujibu wa sheria ndogo zitakazotungwa kutokana na Katiba lakini tunaona Mdude analetwa leo tangu siku anakamatwa yaani wiki mbili zaidi baadaye kitendo ambacho si cha kistaarabu katika nchi ambayo ni huru imesaini mikataba mingi ya kimataifa kuhusu raia na usimamizi wa haki za binadamu si kitendo chema tusingependa kirudiwe", ameeleza wakili Sambwe Shitambala Mwalyego.


Ikumbukwe Mdude Nyagali Mpaluka alikamatwa na jeshi la Polisi mkoa wa Songwe mnamo Novemba 22, 2024 huko wilaya ya Mbozi mkoani humo, akidaiwa kuhusika na makosa ya kusambaza taarifa za uongo mitandaoni, kutoa lugha za matusi na kujeruhi na baadaye ijumaa hii (Desemba 06, 2024) amefikishwa mbele ya mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Songwe na kusomewa shtaka la kusambaza taarifa za uongo mitandaoni kisha kudhaniniwa na wadhamini wawili wenye kuwa barua za utambulisho kutoka kwenye maeneo yao, wawe nyaraka za mali zisizohamishika (bond) zenye thamani ya shilingi million tano kila mmoja.


Kesi hiyo imeahirishwa hadi itakapokuja tena mbele ya mahakama hiyo na ikumbukwe mawakili hao wakiongozwa na Boniface Mwabukusi na Philip Mwakilima walikuwa na maombi mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Mbeya wakiomba Mdude Nyagali adhaminiwe au afikishwe mahakamani hivyo mawakili hao waliokuwa waleta maombi, wameondoa shauri hilo mahakamani mbele ya jaji Victoria Nongwa na mawakili wa Serikali Dominic Mushi na Lodgard Eliaman.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI