MKUU wa Wilaya ya Kibaha Nickson John anatarajiwa kufungua soko la kisasa (Kibaha Shopping Mall) ya Halmashauri ya Mji Kibaha lililogharimu kiasi cha shilingi 8.
Soko hilo ambalo ni la Halmashauri Halmashauri ya Mji Kibaha litatoa fursa za wananchi kukuza kipato chao kwa kufanya biashara mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Kibaha ofisa masoko wa soko hilo la kisasa Sabrina Kikoti amesema kuwa soko hilo limejengwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu na Halmashauri ya Mji Kibaha.
Kikoti amesema kuwa huduma zote zitapatikana ambaapo bidhaa zitauzwa kwa bei ya jumla na rejareja litafungua fursa kwa wananchi wa Kibaha na litatoa ajira na kufufua uchumi wa Kibaha.
Naye ofisa mapato wa Halmashauri ya Mji Kibaha Luna Kakuru amesema kuwa jengo hilo la kibiashara lina maduka 74 ya biashara ambapo bidhaa zitauzwa kwa bei ya jumla na rejareja.
Nao baadhi ya wafanyabiashara Charles Chandika amesema kuwa ametumi fursa kupangisha hapo ili aweze kufanyabiashara ambapo pia litachangamsha Mji wa Kibaha ambapo lengo ni kuhakikisha wanatoa huduma bora na za kisasa na kuwafikia wananchi.
Naye Lydia Vicent ambaye amenufaika kwa kuchangamkia fursa ambapo alikosa sehemu ya kufanyia biashara na wanampongeza Rais kwa kuwapatia fursa wafanyabiashara ambapo fedha zilizotolew ana serikali zimefanikisha kujenga soko hilo.
mwisho.








0 Comments