Header Ads Widget

BALTAZARY WA IWUNGILO AMUUA MWANAMKE NA KUMTOA UTUMBO

  


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Matukio ya ubakaji,Mauaji,Kuvunja nyumba na kuiba yameendelea kuwa tishio kwa wakazi wa Njombe ambapo jeshi la Polisi limeahidi kuchukua hatua kali kuyakabili.

Katika Mkutano na wanahabari Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga amesema wamewakamata watu 48 kwa matukio mbalimbali ya kihalifu,Mauaji na Makosa ya Barabarani katika kipindi cha mwezi mmoja.

Aidha Kamanda Banga amesema matukio ya mauaji yameendelea kupungua ukilinganisha na kipindi kilichopita licha ya kuwapo kwa baadhi likiwemo la Baltazary Sonyonda mkazi wa Iwungilo kumtoa Utumbo mwanamke Mariam Clarence Mdindile kwa kumuingizia mkono katika sehemu ya Haja kubwa baada ya kumtongoza kwa muda mrefu bila mafanikio.

Aidha Wananchi mkoani Njombe Akiwemo Joseph Mgimba na Augustino Mtweve wanasema bado kuna uzembe kwa jeshi la Polisi katika doria wanazofanya hasa majira ya usiku kwani hawaoni Askari wakiwa doria tofauti na miezi kadhaa iliyopita jambo linalosababisha uhalifu kuendelea.

Wamesema mara nyingi Polisi wamekuwa wakionekana wanafanya doria wakati wa siku kuu au yanapotokea matukio makubwa ya ujambazi,mauaji ndipo zinapofanyika doria.

Nao viongozi wa dini mkoani Njombe akiwemo Mchungaji Sephania Tweve anasema wameendelea kuwahubiria mema wananchi ili waepukana na maovu ukiwa ni wajibu wao katika kuirekebisha Jamii.

Hata hivyo Polisi wanatoa wito kwa wananchi na madereva kuwa makini katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kutokana na Historia ya kuwapo kwa matukio mengi wakati wa Siku kuu za Krismas na Mwaka mpya.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI