Header Ads Widget

ASKARI POLISI HUYU NA MGAMBO WASAKWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI IRINGA

NA ZUHURA ZUKHERY, MATUKIO DAIMA, IRINGA

Jeshi la polisi mkoani Iringa linawasaka askari  namba F. 4987 sajent rogas wakituo cha police Ipogolo na askari wa jeshi la akiba Mgambo Thomas Mkembela kwa tuhuma za kumuua Nashon Kiyeyeu (23) mkazi wa nyamhanga kata ya kitwiru Manispaa ya iringa.


Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Iringa SACP Allan Bukumbi alisema kuwa mauaji hayo yametokea Disemba 14 mwaka huu ambapo sajent Rojas kwa kushirikiana na mgambo walimkamata mtuhumiwa Nashon Kiyeyeu kwa tuhuma za kuiba simu na kudaiwa kumpiga mtuhuniwa huyu hadi kupoteza fahamu .

Alisema kuwa sajent Rogers alipokea taarifa kutoka kwa mwananchi mmoja ambaye hakumtaja jina kuwa anamtuhumu Nashon Kiyeyeu amemuibia simu, ndipo sajent Rogers kwa kushirikiana na mgambo Thomas Mkembela walimkamata mtuhumiwa .

Marehemu enzi za uhai wake 

Kamanda SACP Allan Bukumbi alisema baada ya kumkamata wanadaiwa kumpiga mtuhumiwa huyo walipoona amepoteza fahamu wakampeleka hospitali binafsi na baadaye wakampeleka Hospital ya Rufaa ya Iringa na ikabainika mtuhumiwa huyo amefariki dunia.

Alisema kuwa baada ya kuona mtuhumiwa huyo amefariki kutokana na kipigo walitoweka wasikojulikana ambapo jeshi la polisi mkoa wa Iringa linaendelea na msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa hao pamoja na kusambaza taarifa mikoa mbalimbali.

SACP Allan Bukumbi ametoa wito mtu yeyote atakayemuona sajent Rogers na Mgambo Thomas Mkembela watoe taarifa wakamatwe na hatua zingine za kisheria zifuate.

SACP Bukumbi aliesema kuwa jeshi la polisi mkoani Iringa halita sita kumchukulia hatua za kisheria mtu yoyote ambaye ataonekana kuvunja sheria.


Kwa upande wake baba mzazi wa kijana aliyeuawa mikononi wa asikari huyo Lusia Kiyeyeu alisema alipata taarifa kutoka kwa dada yake alikokuwa anafanya kazi kuwa Nashon amekamatwa na polisi anaelekea kituo cha polisi Ipogolo.

Alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo alifuatilia kituoni hapo hakumkuta kijana wake wala askari aliemkamata na baada ya kuuliza ikaonekana hakufunguliwa jarada kituoni hapo.

Kiyeyeu aliongeza kuwa baadae alifika kituo kikuu cha mkoa wa Iringa lakini pia hakufunguliwa jarada katika kituo hicho.

Naye dada yake Nashon  alisema kuwa kabla ya tukio alimtuma kijana huyo akamuombee chenji benki ya na aliporudi alimuomba ruhusa bosi wake aende kuchukua simu kwa fundi huku nyuma wakaja watu na gari kumuulizia kijana huyo.

TAZAMA FULL VIDEO YA MAUAJI BOFYA LINK HII

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI