NA HADIJA OMARY
LINDI.
Jamii imehaswa kuwa na utaratibu wa kujitolea na kutoa msaada kwa Watu wenye uhitaji ili kueneza upendo kwa wasionacho na kujiona wapo sawa
Wito huo umetolewa na mkurugenzi wa LECO lishe Imelda Gama alipotembelea na kutoa msaada wa unga lishe, daipas, juice na sukari kwa watoto na akina mama waliojifungua katika hospital ya Rufaa mkoa wa Lindi Sokoine ikiwa ni sehemu ya kusheherehekea siku yake ya kuzaliwa
Wazazi waliopatiwa msaada huo akiwemo Merry Hussein walimshukuru mdau huyo kwa msaada alioutoa wakitoa wito kwa Wadau wengine kuiga kutoka kwake
Betrida Mwaikambo na Issa Ngasha ni wakazi wa Manispaa ya Lindi wamempongeza mkurugenzi huyo kwa uamuzi wake wa kutumia siku yake hiyo ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake kukumbuka kundi hilo muhimu
" Tumeshuhudia Watu walio wengi wamekuwa wakisheherehekea siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwao Katika mambo ya starehe lakini Dada huyu amekuwa wa tofauti na hao kwa kweli Jamii tunakitu cha kujifunza kutoka kwake.
Amesema mara kadhaa ujiwekea utaratibu wa kuwakumbuka watoto, Wazee, na wafungwa Katika kumbukizi ya siku yake hiyo ya kuzaliwa ili kuwa pamoja na makundi hayo muhimu kwa Jamii
" Nimefukiria kuja huku kwa sababu Mimi ni mama hivyo natambua matatizo wanayoyapata akina mama wenzangu hasa katika utokaji wa maziwa hivyo kwa unga huu wa LECO ambao unavirutubisho mbalimbali unamuwezesha mama anaenyonyesha kutengeneza maziwa ya kutosha"
Amesema kupitia juice ya LECO iliyotengenezwa kwa kutumia bitrut na lozela inaongeza Damu, zink na calcium ni mzuri kutumiwa na rika zote na jinsia zote
Evadia masota ni daktar wa watoto Katika hospital ya Rufaa mkoa wa Lindi Sokoine Amesema kutokana na vitu mbalimbali vilivyochangavywa kwenye unga lishe huo unamuwezesha Mtoto na mama anaenyonyesha kupata virutubisho vya kutosha
" Kwa kuangalia unga lishe huu unamchanganyiko wa vitu mbalimbali, tunaona bitrut , Mbegu za maboga, mahindi lishe na soya isiyokobolewa , virutubisho hivyo vyote ni vizuri na vinafaa kwa matumizi hasa kwa wamama wanaonyonyesha"








0 Comments