Header Ads Widget

ABDUL NONDO APATIKANA AKIWA MAHUTUTI

Mwenyekiti wa ngome ya Vijana ya Chama cha ACT Wazalendo Abdul Nondo amepatikana Usiku huu ambapo inaelezwa ameokotwa katika eneo la ufukwe Coco na baadaye kuletwa katika ofisi za Chama hicho na watu ambao bado hawajajulikana, na amekimbizwa Hospitali ya aga Khan kutokana na majeraha aliyokutwa nayo mwilini mwake.


Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amesema kuwaMwenyekiti huyu  wa Ngome ya Vijana wa chama hicho, Abdul Nondo amepatikana usiku huu wa leo Jumapili, Desemba 1, 2024.

Nondo alichukuliwa na watu wasiojulikana alifajiri ya leo stendi ya mabasi Magufuli aliposhuka kwenye basi akitokea mkoani Kigoma, na amekutwa akiwa ametupwa pembeni mwa makao makuu ya chama hicho yaliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam.

Mwananchi limezungumza na Ado ambaye amesema kwa kifupi ni kweli amepatikana.

Taarifa zimedai Nondo ametupwa na watu wasiojulikana ofisini na hali yake si nzuri na akiwa hajitambui.

Matukio Daima media tunaendelea kufuatilia zaidi tutakukuza 

TAZAMA FULL VIDEO BOFYA LINK HII

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI