Na. Matukio Daima App,Dar
Wasanii wa Tanzania ( Magoma Moto) na wasanii wa China wanaupamba usiku wa Tanzania na China katika kilele cha kufunga rasmi maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China, na uzinduzi wa Filamu ya Amazing Tanzania.
Filamu ya Amazing Tanzania iliyowashirikisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, na mwigizaji mahiri kutoka China Bw. Jin Don imeleta mafanikio makubwa katika kipindi kifupi tangu izinduliwe nchini China mapema Mei mwaka huu.
0 Comments