Header Ads Widget

TANGANYIKA TEAM YATAMBA KUFANYA VIZURI KLABU BINGWA KIKAPU

 Na Fadhili Abdallah,Kigoma

TIMU ya mpira wa kikapu ya L Tanganyika Basket Ball ya mkoa Kigoma inaanza safari jioni ya November nane kuelekea mkoani Dodoma kwa ajili ya mashindano ya klabu bingwa Tanzania ya mchezo huo huku ikitamba kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.

Katibu wa timu hiyo ambaye pia ni Kocha,  Anastas Kibonajoro alisema hayo mbele ya Mkuu wa mkoa Kigoma, Thobias Andengenye wakati akikabidhi kombe la Taifa Cup kwa Mkuu huyo wa mkoa na kusema kuwa waliyofanya kwenye Taifa Cup watafanya pia kwenye mashindano hayo ya Klabu Bingwa nchini.

Pamoja na hivyo Katibu huyo alisema kuwa wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa fedha kwa ajili ya kugharamia mambo mbalimbali kwenye michuano hiyo hivyo kuomba wadau mbalimbali ndani na nje ya mkoa Kigoma kujitokeza kuwasaidia.

Akizungumza wakati akipokea kikombe cha mashindano ya Taifa Cup ambacho timu ya mkoa Kigoma ilishinda Mkuu wa mkoa Kigoma ameipongeza timu hiyo kwa ushindi huo ambao umeleta heshima kubwa kwa mkoa na kuweka ramani ya mkoa kwenye mchezo wa mpira wa kikapu.

Sambamba na hilo Mkuu huyo wa mkoa ameitaka timu ya  Tanganyika Basket Ball  ambayo ilitumia nafasi hiyo kuomba baraka za mkoa kuelekea mashindano kufanya vizuri ikichangiwa kiasi cha shilingi milioni mbili taslimu huku ofisi ya Katibu Tawala wa mkoa Kigoma ikitoa shilingi milioni.

Naye Katibu Tawala wa mkoa Kigoma,Hassan Ruga Pamoja na ofisi yake kutoa kiasi cha shilingi milioni moja kuchangia maadnalizi ya timu hiyo amesema kuwa wataendelea kutafuta namna ya kutafuta misaada Zaidi ili kuiwezesha timu hiyo iweze kupata huduma muhimu na kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI