IRUWASA inatarajia kufanya maboresho kwenye Mfumo wa mita za maji za Malipo kabla (LUKU) kuanzia tarehe 5 hadi 8/11 2024.
Kufuatia Maboresho hayo, Mteja wa Mita ya malipo kabla utatumiwa TOKENI ambazo utaingiza katika mita yako ya maji kabla ya kuingiza TOKENI za maji.
Kufuatia zoezi hili, IRUWASA inawaomba
wateja wake wote wa mita za Malipo kabla kununua maji ya kutosha kabla ya kuanza zoezi hilo.
Maboresho yamepagwa kufanyika (*tarehe 5-8/11/2024).
Hii itaepusha usumbufu wa kukosa maji kipindi Maboresho yakiwa yanaendelea.
Atakayepata tangazo hili amjulishe na mwenzie.
IRUWASA inaomba radhi wateja wake wa mita za Malipo kabla kwa usumbufu wote utakaojitokeza.
0 Comments