Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Wananchi Wamehamasishwa Kujitokeza Kwenda Kuwachagua Viongozi wa Serikali za Mitaa Ambao Watawaongoza Kwa Kipindi cha Mika Mitano Ijayo Baada ya Serikali Kuweka Mazingira Rafiki ya Kupiga Kura Kwa Watu Wote Wenye Sifa ya Kufanya Hivyo Wakiwemo Walemavu Huku Shughuli zote za Serikali Sikisitishwa Ili Kuruhusu Wananchi Kwenda Kushiriki zoezi Hilo Muhimu.
Waziri wa Mali asili na Utalii Balozi Dokta Pindi Chana ni Miongoni Mwa Viongozi Walio Zungumza na Wananchi Mjini Njombe Katika Soko kuu ambapo Amewataka Wananchi Kwa Umoja Wao Kwa Vyama Vyote vya Siasa Kutumia Siku Hiyo Maalumu Kwenda Kupiga Kura.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka Amesema Serikali Imechagua Siku ya Kazi Kuwa ya Mapuziko toafauti na Hapo Awali Lengo ni Kutoa Nafasi Kwa Wananchi Wote pasina Kujalisha Taasisis za Kidini Ili Kushiriki Uchaguzi Huo.
Pia Mtaka amewahakikishia wananchi ulinzi wa kutosha katika vituo vyote vya kupigia kura hivyo wanapaswa kwenda kwa amani kuwachagua viongozi wanaowataka.
Baadhi ya Wananchi Kutoka Mjini Njombe Wamekiri Kwenda Kuwachagua Viongozi wao Ambao Wata Waongoza Kwa Kipindi cha Miaka Mitano Ijayo Huku Wakitoa Wito Kwa Wananchi Wengine Kuto Puuza Jambo Hilo Kutokana na Umuhimu Wake.
0 Comments