Na,Jusline Marco;Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda leo amewahimiza wananchi wa jiji la Arusha kujenga utamaduni wa kufanya usafi mara kwa mara kwenye maeneo yao ya kazi na kwenye makazi yao ili kufanya mandhari ya Mkoa huo kuvutia zaidi wageni na watalii.
Akiwaongoza wananchi wa jiji la Arusha kwenye zoezi la Ufanyaji wa usafi katika maeneo mbalimbali,Makonda ikiwemo katika Soko la Kilombero, Makonda amewakumbusha wananchi hao pia kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la upigaji kura za kuchagua Viongozi wa serikali za mitaa hapo Kesho Novemba 27, 2024, ambapo tayari Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa siku ya mapumziko ili kuwaruhusu wananchi kushiriki kikamilifu katika upigaji kura.
Pamoja na hayo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Felician Mtahengerwa na Meya wa Jiji la Arusha Maximillian Iranghe kuanza mara moja kutatua changamoto za kutuama kwa maji ndani ya soko la Kilombero wakati wa msimu wa mvua pamoja na kuvuja kwa paa la soko hilo.
0 Comments