Header Ads Widget

MADAKTARI BINGWA WA MAMA SAMIA KUTOA HUDUMA KWA WAKAZI WA NJOMBE HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA NJOMBE

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Wizara ya afya imepanga kuendelea kuwasaidia wananchi kwa kuwapa huduma za kibingwa kupitia Madaktari bingwa wa Mama samia ambapo safari hii Kanda ya Nyanda za Juu kusini italetewa Madaktari hao katika Hospitali za Rufaa kuanzia mwezi Disemba.



Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Njombe Dokta Gilbert Kwesi mbele ya Vyombo vya habari anasema Miongoni mwa Magonjwa yatakayotolewa huduma  kupitia  Madaktari hao ambao wataweka kambi kuanzia Disemba 2 hadi 6 mwaka huu ni pamoja na Saratani,Ubongo,Moyo,Upasuaji pamoja na  mifupa.


Wananchi mkoani Njombe akiwemo Grace Chengula na Francis Nindi wanasema ujio wa Madaktari hao utakwenda kuwa mkombozi hususani kwa wasio na kipato kikubwa licha ya kuwa huduma zitatolewa kwa kuchangiwa.

Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali Hiyo Asilimia 16 ya wagonjwa waliolazwa katika kipindi cha mwaka huu ni waliotokana na ajali za magari,Pikipiki na Bajaji huku akiziomba mamlaka husika kuelekeza nguvu ya utoaji elimu kwa madereva.


Wakazi wa Njombe wanaelekeza lawama kwa Madereva kwamba wengine wamekuwa walevi na wazembe na kuwataka kuwa makini pindi wawapo barabarani.

Kwa upande wao baadhi ya madereva Bodaboda mjini Njombe akiwemo Levinyo Benedict na Deus Sanga wanatupia lawama ubovu wa miundombinu ya barabara na kwamba zimechimbika na ni nyembamba zinazowasababishia ajali.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI