Header Ads Widget

KAMPENI ZIMEISHA KWA AMANI : ANDENGENYE

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MKUU wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye amesema kuwa hakuna vurugu au uvunjifu wa amani uliojitokeza wakati za zoezi la kampeni kwa vyama vya siasa kuelekea uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake mjini Kigoma Novemba 26 mwaka huu Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa vyama vyote vya siasa na wagombea wake walipewa nafasi sawa ya kufanya kampeni na kunadi sera zao ambapo vyama 17 vimeshiriki kwenye mchakato huo wa kampeni.

 

Andengenye alisema kuwa hawajapokea malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa, wala wagombea kuhusu kuzuia kufanya kampeni au kufanyiwa kuvuru au aina yeyote ambayo imeathiri kampeni zao na kwamba serikali imejipanga kuimarisha amani na urulivu wakati wa kupiga kura na kutangaza matokeo kama ilivyokuwa kwenye zoezi la kampeni.

 

Kwa upande wao Taasisi ya kuzuia na kupamba na rushwa (TAKUKURU) mkoa Kigoma imesema kuwa vitendo vya rushwa vimeendelea kujitokeza kwenye uchaguzi huo lakini taarifa walizokuwa wakipewa na raia wema zimesaidia kuzuia vitendo hivyo wanapovamia eneo husika na wanatuhuma na jambo hilo kukimbia ingawa hakuna aliyekamatwa hadi sasa.

 

Mkuu wa TAKUKURU mkoa Kigoma, John Mgallah akizungumza na waandishi wa Habari mjini Kigoma jana alisema kuwa semina na mikutano waliyoendesha kwa wadau mbalimbali kuhusu kuzuia na kupambana na rushwa kwe ye uchaguzi huu imesaidia kupata taarifa nyingi ambazo wamekuwa wakizifanyia kazi na kwamba japo hawajakamata mtu yeyote lakini vitendo vingi vya rushwa vimezuiwa.

 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI