Na Fadhili Abdallah,Kigoma
MKUU wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye ameitaka Wakala wa maji mijini na vijijini (RUWASA) kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM inayoitaka wakala huo kuhakikisha upatikanaji wa mkoa mkoani Kigoma unafikia asilimia 85 ifikapo Juni 2025.
Andengenye alisema hayo akikabidhi gari moja aina ya Toyota Hilux Vigo kwa Meneja wa RUWASA mkoa Kigoma na kusema kuwa upatikanaji wa vitendea kazi kwenye sekta ya maji lazima vijibu mpango wa Raisi Samia wa kumtua mama ndoo.
Alisema kuwa mkoa umefanya kazi nzuri ya utekelezaji wa miradi ya maji tangu Raisi Samia alipoingia madarakani ambapo upatikanaji wa maji kwa wananchi umeongezeka kutoa asilimia 58 na kufikia asilimia 74 iliyopo sasa ambapo ametaka miradi 39 iliyopo kwenye mpango itekelezwe kuhakikisha upatrikanaji maji kwa wananchi unaongezeka.
Akizungumza katika makabidhiano hayo Katibu Tawala wa mkoa Kigoma Hassan Ruga alisema kuwa kwao kama ofisi ya Katibu Tawala wa mkoa kunawapa nafasi ya kuwahimiza katika watendaji utekelezaji wa miradi ya maji kutokana na kuwepo kwa nyenzo zinazowafikisha kwenye maeneo ya utekelezaji.
Awali Meneja wa Wakala wa maji mijini na vijijini (RUWASA) Mkoa Kigoma Mhandisi Mathias Mwenda alisema kuwa kwa sasa maji yanapatikana kwa asilimia 74 mkoani Kigoma na kutekelezwa kwa miradi 39 ambayo inatarajia kukamilika Desemba 2025 kutaufanya mkoa huo kufikisha asilimia 87 kwa wananchi wake.
Mwenda alisema kuwa upatikanaji wa gari hilo unaondoa changamoto ya ofisi ya meneja wa RUWASA mkoa Kigoma kuomba gari kwa Meneja wa RUWASA wilaya Uvinza hivyo kuathiri utendaji kazi katika wilaya hiyo.
0 Comments