Header Ads Widget

MWALIMU ADAIWA KUMLEWESHA NA KUMBAKA MWANAFUNZI WAKE


Na Shemsa Mussa 

MULEBA ,KAGERA.

MTOTO miaka( 13) Tuombe Aman (jina lake sio halisi) mkazi wa kijiji cha Rulanda Kata Rulanda wilayani Muleba mkoani Kagera mhitimu wa darasa la saba shule ya msimgi Rulanda anaeleza yaliyomkuta baada ya kuambiwa arudi shuleni kupewa ushauri juu ya matokeo ya mitihani yake.

Tuombe ameaeleza kwamba octoba 30 mwaka huu,alienda shuleni hapo baada ya kuwa amesikia kwamba matokeo ya darasa la saba mwaka huu yametoka akawa na shauku ya kufahamu ufaulu wake.

Majira ya saa 9:00 alasiri alienda shuleni kuonana na mwalimu wa taaluma aitwae Lameck Jonas ili aweze kuangalia matokeo endapo amefaulu aliweza kuangalia na kukuta akiwa na ufaulu wa daraja D

Mwalimu wa taaluma Jonas akamwambia arudi majira ya saa 10:jioni ili ampatie ushauri,Tuombe aliondoka na kurudi nyumbani ili asubili muda alioambiwa na mwalimu wake ufike.

Tuombe alisema ilipofika majiara ya10: 00jioni  ariludi shuleni hapo ili aupokee ushauri wa mwalimu na wakati anasubili mwalimu wake afikie aliingia katika darasa ambalo alikuwa akisoma na wenzake kwa lengo la kumsubili mwalimu.

Alisema baada ya muda mwalimu alifika shuleni hapo na kuingia katika darasa alilokuwa amekaa Tuombe akaamza kufunga madirisha na mlango nakisha kumwambia Tuombe avue nguo alizokuwa amevaa.

"Nilikataa kuvua akanifungua zipu na akaamza kunipaka mafuta,shingoni, mgongoni,kwapani, kwenye matiti na sehemu za siri alafu akaniweke vitu kama sukari mdomoni na akanipa na maji ninywe nikakataa akanilazimisha sijui vilikuwa madawa ya kulevya sikujua kilichoendelea" anaeleza Tuombe

Baadae na mwalimu alivua nguo zote sawa na mtu anaeenda kuoga ,ndipo akachukua mafuta mengine akanipaka tena sehemu za siri sikuona kilichofanyika akaona mwalimu huyo  akichungulia katika madirisha sawa na mtu ambae anaangalia watu nje ndio akaniambia niende nyumbani

"Nilivotoka nje akaniita akasema ludi nikaludi akaniambia baba na mama wakiniuliza nilikuwa wapi niseme  nilikuwa kwa rafiki yangu,alafu wakiniuliza mbona mdomo umekauka niseme ndivo nilivo, wakiniuliza mbona unatembea hivo nisema kwamba ndio ninavyotembea au nilianguaka chini"aliendele kuelezea 

Alisema kuwa mwalimu wa taaluma alimwabia endapoa ataendelea kusikia maumivu amwambie mdogo wake aende kwa mwalimu huyo amwelezee tatizo hilo ili aone atawezaje kumsaidia.

Mama wa mtoto huyo majina yake yamehifadhiwa alisema, ilipofika majira ya 11:00jioni bila ya kuona mwanae aliamua kwenda shuleni kumtafuta hakuna mtu yoyote bali pikipiki iliyokuwa nje akawawaza atakuwa ameenda wapi.

Alisema na pikipiki iliyokuwa nje alizoe kwamba watu huwa wanaacha eneo hilo na kwenda,kufuata samaki ziwani hivyo hakuwaza kwamba kutakuwa na mtu mazingira ya shule hiyo.

Alisema ilipofika majira ya 1:30 mtoto alifika nyumbani ndipo alihoji na kuanza kuelezea kwamba mwalimu wake alikuwa amemfungia .

Alisema baada ya kuona hali hiyo familia ilichukua hatua ya kwenda kutoa taarifa kwenye uongozi wa kijiji kwa mtendaji ili waweze kusaidia tukio hilo.

Baada ya siku wiki Moja walikuja ndug na jaman katika familia hiyo ili waweze kuzungumza yaweze kuisha na mwalimu aludi kazini kwani ni wiki mbili sasa haonekani

"Walikuja ndugu zake eti tuzungumze na watupe pesa yaweze kuisha na mwalimu aludi kazini  nikawajibu kama munaona ndugu yenu aludi kazini je Mimi mama mtoto ninajisikiaje kufanyiwa kitendo hiki mwanangu!?"alisema Mama wa mtoto.

Jirani wa familia hiyo Winston Joseph alisema siku ya tukio aliambatana na baba wa familia kwenda kwa mtendaji wa kijiji kutoa taarifa za ukatili aliofanyiwq mtoto.

Alisema walipofika kwa mtendaji walipewa usafiri wa kwenda hospitali ya Kaigara kwa ajili ya vipimo na kupewa barua ya kwenda kituo cha jeshi la polisi kupatiwa PF3 ya matibabu.

"Nikiwa kama mzazi ninaumizwa sana na matumio ya ubakaji ukiqngalia kwa umri watoto huyu bado ni mdogo anandoto anandoto zake"alisema Joseph 

Aliongeza jamii inaamimi kwamba mwalimu nao ni sehemu ya wazazi katika malezi hii hali itafanya kutowaamini na kuwa na hofu ya kusomesha watoto.

Mwalimu mkuu wa shule ya Rulanda alikiri kutoka kwa tukio hilo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI