Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Serikali kupitia wizara ya kilimo imeipa wilaya ya Njombe matrekta matano kwa ajili kutekeleza mradi wa Jenga kesho iliyobora[BBT]Uliyoibuliwa na mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa na kisha vijana zaidi ya elfu 8 kuchangamkia fursa za kilimo,Ujasiriamali na biashara ambazo zitakuwa zikitolewa katika halmashauri zote tatu za wilaya hiyo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya matrekta hayo yaliyotolewa na wizara ya kilimo kwa ajili ya kutekeleza mradi BBT Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa na katibu tawala Aghatha Mhaiki wameishukuru wizara kuona umuhimu wa kuipa wilaya hiyo Matrekta kwa ajili ya uzalishaji mkubwa unaofanywa katika kilimo na kwamba mitambo hiyo itakuwa ikikodishwa pia kwa wananchi kwa bei nafuu ili kufanya mapinduzi ya kilimo na uchumi.
Awali Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Njombe Kuruthumu Sadick na Thadei Luoga Ofisa Kilimo na Uvuvi wamesema kitendo cha serikali kutoa matrekta hayo itakuwa chachu ya kufanikisha miradi ya Jenga Kesho iliyo bora BBT na kisha kuweka wazi vitu vingine vilivyoletwa .
Kwa upande wao wananchi kutoka maeneo tofauti ya mji wa Njombe akiwemo Elisha Figawa na Tea Haule Wanasema matumizi ya teknolojia katika kilimo yataongeza ufanisi na kuokoa muda huku pia wakitaka mbolea kupunguzwa bei na dawa za mazao.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Mhe.Kissa Gwakisa Kasongwa
Ujio wa zana hizo za Kilomo utakwenda kusaidia kupunguza changamoto kwa wakulima hasa vijana waliolengwa kwenye mradi wa BBT na kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
0 Comments