Na Jusline Maro;Arusha
Serikali imesema kuwa rasilimali inayosimamiwa vizuri ni tunu ya kuliwezesha Bara la Afrika kufikia kiwango bora cha maendeleo.
Akifungua Mkutano wa 9 wa Mwaka wa Mtandao wa Mameneja na wasimamizi wa Rasilimali watu katika sekta za Umma Barani Afrika unaofanyika jijini Arusha kwa niaba ya Rais Samia, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kasimu Majaliwa Majaliwa amesema mkutano huo utawapa fursa pana washiriki katika kubadilishana uzoefu katika usimamizi wa rasilimali watu kipitia mawasiliano na maandiko kutoka kwa wawezeshaji katika nchi tofauti barani Afrika.
Amesema rasilimali watu katika utumishi wa umma ni nyenzo muhimu na yenye thamani kubwa ambapo serikali husika inaitumia kwa wananchi wake katika kutoa huduma za kijamii, kiuchumi ili kukuza ustawi wa jamii husika.
Akitoa taarifa katika Mkutano huo Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.George Simbachawene amesema kauli mbiu ya mkutano huo inaenda sambamba na changamoto zilizopo ambazo zinahitaji mijadala na kubadilishana mawazo ili kuweza kupata majawabu yanayoweza kujibu masuala magumu yanayopelekea watumishi wa umma wasiweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo
Kwa upande wake Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Katiba na Sheria Utumishi wa Umma na Utawala bora Zanzibar Mhe. Haroon Ali Suleiman kutoka serikali ya mapinduzi Zanzibar,akizungumza katika Mkutano huo amesrma amani na muungano uliopo kati ya serikali ya mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhurj ya Muungano wa Tanzania ndiyo itakayowezesha maendeleo kuzidi kusonga mbele na kuleta matokeo makubwa zaidi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Monduli Festo Shemu Kiswaga akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amesema viongozi wa rasilimali watu wanapaswa kuwa na mbinu za kisasa zinazojumuisha maarifa,uadilifu na ufanisi katika kujenga watumishi wanaoweza kustahimili na kubadilika na changamoyo zinazokwenda na mabadiliko ya teknolojia za mahitaji ya kiuchumi kwenye nchi za Afrika.
Kauli Mbiu katika Mkutano huo ni Utawala stahimilivu na Ubunifu Kutunza sekta ya Umma ijayo kupitia Uongozi wa Rasilimali watu.
0 Comments