Header Ads Widget

AIBU BOSS WA ANIF AKUTWA NA VIDEO HIZI ZA NGONO

 


Katika hali isiyokuwa ya kawaida na isiyotarajiwa Baltasar Ebang Engonga (54) ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Upelelezi wa Fedha (ANIF) la nchini Equatoria Guinea, kwa sasa yuko katikati ya kashfa kubwa baada ya mamlaka za kiinterejensia nchini humo kugundua mamia ya video za utupu zinazodaiwa kumuonyesha Mkurugenzi huyo akifanya mapenzi/ ngono na wanawake tofauti tofauti


Inasemekana kuwa, video hizo zinajumuisha matukio na watu mashuhuri, kama vile mke wa kaka yake, binamu yake, na dada wa Rais wa Equatorial Guinea


Kashfa hiyo imejitokeza wakati wa uchunguzi wa ulaghai, ambapo inaelezwa kuwa wachunguzi wamepata zaidi ya video 300 kwenye kompyuta ya Ebang Engonga mwenye umri wa miaka 54, zinazoonyesha matukio na wanawake mbalimbali wakiwemo wengine walioolewa



Video hizo ambazo zinadaiwa kupatikana katika ofisi yake binafsi, inasemekana zimerekodiwa kwa ridhaa yake na zimevuja mtandaoni, na kusababisha msukosuko na na mjadala mkubwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na yombo vya habari ndani na nje ya nchi hiyo


Makamu wa Rais wa Equatorial Guinea Teodoro Nguema, amezungumzia kashfa hiyo katika taarifa ya umma iliyochapishwa kupitia mtandao wake binafsi wa X (twitter) ambapo amelaani vikali mienendo isiyofaa ndani ya ofisi za serikali/ umma


Makamu huyo wa Rais amesisitiza kuwa mahusiano ya kimapenzi hayaruhusiwi kabisa katika maeneo ya utawala na pia ameonya juu ya adhabu kwa wale watakaokiuka


"Kutokana na matumizi mabaya yaliyoonekana kwenye mitandao ya kijamii nchini Equatorial Guinea siku za hivi karibuni, na kwa kukumbuka kuwa Wizara na taasisi za serikali ziko kwa ajili ya kufanya kazi za utawala pekee, kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya nchi, mahusiano ya kimapenzi katika ofisi yamepigwa marufuku" -Nguema


"Mbinu za udhibiti zipo tayari, na yeyote atakayekiuka kanuni hii tena atachukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa tabia isiyofaa na atafutwa kazi mara moja" -Nguema


Lakini unaweza kujiuliza Baltasar Ebang Engonga ni nani? Baltasar, huyu ni Mkurugenzi Mkuu wa ANIF, ambalo ni Shirika la Kitaifa la Upelelezi wa Fedha la Equtorial Guinea, ambapo majukumu yake yanajumuisha kusimamia uchunguzi wa kifedha na kusimamia shughuli zinazolenga kudhibiti ufisadi wa kifedha nchini Equatorial Guinea

Inaelezwa kuwa Bartasar ameoa na ana watoto sita, huyu anatajawa kushikilia nafasi muhumu katika shirika hilo ambalo lina ushawishi mkubwa juu ya uwazi wa kifedha na mfumo wa udhibiti wa Taifa

Kama hiyo haitoshi, jambo la kushangaza zaidi ni kwamba baadhi ya matukio yametokea katika ofisi yake ya kazi, ikiwemo wakati ambapo anaonekana akiwa amelala na mwanamke kando ya bendera ya Taifa hilo


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI