Header Ads Widget

MNEC QWIHAYA ASIFU ZOEZI LA UCHAGUZI ,AWAPONGEZA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI

 

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Leonard Mahenda Qwihaya, maarufu kama Manguzo, leo tarehe 27 Novemba 2024, ameshiriki katika zoezi la kupiga kura kuchagua viongozi wa serikali za mitaa, vijiji, na vitongoji. 

Zoezi hilo limefanyika katika mtaa wa Kabambo, kata ya Kiseke, wilaya ya Ilemela, mkoani Mwanza.

Baada ya kushiriki katika zoezi hilo, MNEC Qwihaya amewapongeza wakazi wa eneo hilo kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika kupiga kura. 

Alisisitiza umuhimu wa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi waliowachagua kwani  ni viongozi watakao waletea maendeleo .

Aidha, Qwihaya amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kusimamia demokrasia kwa kuagiza matokeo ya uchaguzi yatangazwe kama yalivyoamuliwa na wananchi kupitia sanduku la kura.

 

Alisema hatua hiyo inadhihirisha nia ya dhati ya Rais Samia ya kudumisha demokrasia ya vyama vingi nchini.

Kwa mujibu wa Qwihaya, uchaguzi huu ni ishara ya uimara wa misingi ya demokrasia nchini, ambapo wananchi wanapata fursa ya kuchagua viongozi wanaowaamini.

 Aliwahimiza Watanzania wengine kuiga mfano wa wakazi wa Kabambo kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi.

Qwihaya pia alisisitiza kwamba kiongozi wa kweli ni yule anayeheshimu matakwa ya wananchi na kuyasimamia. Alitoa wito kwa viongozi wote wanaochaguliwa kuhakikisha wanawatumikia wananchi kwa uadilifu, uwazi, na kwa kutanguliza maslahi ya taifa. Alimalizia kwa kuwapongeza waandaji wa uchaguzi kwa kuhakikisha mchakato mzima unakuwa huru na wa haki.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI