Header Ads Widget

MGOMBEA WA CHADEMA ALIYEENGULIWA ASHINDA UENYEKITI WA KIJIJI..


 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro kimeeleza kushangazwa na Mgombea wake katika Kijiji cha Useri, Kata ya Machame Narumu, Wilfred Ritte kutangazwa mshindi wa nafasi ya uenyekiti wa kijiji hicho, licha ya kuondolewa katika kinyang'anyiro katika hatua za mapingamizi.

Katika matokeo hayo mgombea huyo wa Chadema anaonekana kupata kura 428 huku wa CCM akipata kura 408.

Akizungumza kwa njia ya simu  Katibu wa Chadema Wilaya ya Hai, Joseph Ntele amesema moja ya maajabu na miujiza waliyoiona katika uchaguzi wa serikali za mitaa ni mgombea huyo kutangazwa mshindi licha ya kuondolewa katika hatua ya mapingamizi na hakushiriki kampeni wala kuweka wakala katika kituo hicho.

"Kata ya Machame Narumu ni moja kati ya kata ambazo wagombea wetu kwa zaidi ya asilimia 99 walienguliwa na miongoni mwa walioenguliwa ni Ritte. Mgombea alikata rufaa kupinga maamuzi ya msimamizi msaidizi wa uchaguzi wa Kijiji cha Usari na Kamati ya Rufani ilitupilia mbali malalamiko yake.

"Katika hali ya kushangaza na kustaajabisha tumeona kwamba ameshinda nafasi ya uenyekiti wa kijiji hicho, na katika kituo cha kupiga kura wenyewe hatukuwa na mawakala na hatukufanya kampeni kwa sababu mgombea alienguliwa."

Akizungumza kwa njia ya simu, kuhusiana na suala hilo, Msimamizi wa Uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Hai, Dionis Myinga amesema hajapokea lalamiko hilo kwa maandishi wala kutoka kwa Chadema, ingawa alikiri kulisikia kutoka kwa viongozi wa CCM wa kata hiyo.

#Chanzo Mwananchi 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI