Header Ads Widget

MGOMBEA UENYEKITI CCM IDUNDILANGA NJOMBE KUPAMBANA NA MIKOPO KAUSHA DAMU

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Changamoto za wanawake Kukimbia familia na kuacha watoto wakiteseka kutokana na marejesho ya mikopo kausha damu zimetakiwa kufanyiwa kazi na viongozi wanaotarajiwa kuchaguliwa Novemba 27 mwaka huu katika uchaguzi wa serikali za mitaa.


Katika Kampeni za uchaguzi huo za Chama cha mapinduzi CCM mtaa wa Idundilanga kata ya Njombe mjini mkoani Njombe Mgombea uenyekiti Elizabeth Mlowe  anasema sambamba na kupanga kufanyia kazi changamoto ya lishe kwa kuwaelimisha akina mama lakini Mikopo kausha damu nayo imekuwa ikimkwaza na kwamba akichaguliwa atakwenda kupigania suala hilo.


Wananchi wa Idundilanga Akiwemo Edina Mbanga wamesema wanataka mwenyekiti ajaye akashughulikie changamoto hiyo ya Mikopo Kausha Damu kwa kuwa Inasababisha madhara makubwa katika familia nyingi mtaani hupo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Njombe mjini Alatanga Nyagawa amesema endapo wananchi watamchagua mgombea wa CCM basi itakuwa rahisi kupigania maendeleo ya wananchi hasa kuelekea katika ujio wa Chuo kikuu cha Dodoma Tawi la Njombe.



Hizo ni sera za wagombea mbalimbali wanazonadi kwa wananchi kupitia mikutano ya kampeni zinazoendelea mkoani Njombe ikiwa Novemba 26 ni tamati ya kampeni Tayari kwa uchaguzi hapo Novemba 27 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI